Kwa 'Wasomi' wetu: Badilikeni, mnatia aibu

Kwa 'Wasomi' wetu: Badilikeni, mnatia aibu

Kainetics

Senior Member
Joined
Jun 20, 2022
Posts
135
Reaction score
276
Niende moja kwa moja kwenye mada ya kichwa cha uzi. Kadri siku zinavyokwenda idadi ya wanaofanikiwa kufaulu mtihani wa kidato cha nne, ule wa kidato cha sita, wale wanao hitimu mavyuoni ambao mwisho wa siku wanakua waajiriwa au wanajiajiri, au wapo tu mtaani, ni kubwa na inayoendelea kukua.

Ila hawa, ambao walipaswa sasa kuwa walau ndiyo wana ile elimu, kuna mambo bado wanayo ambayo yanatia aibu, unajiuliza sasa huyu ndiyo kasomea nini?

Kama unafaa kwenye kipengele kimoja wapo kati ya hizo hapo juu na unafanya yafuatayo, badilika maana sasa hiyo elimu yako ni sawa na kazi bure.

1. Unalipa kutengenezewa e-mail

Nilikua sijui kama na hiki ni kitu ambacho huwa kipo, hadi jana nikiwa nanunua simu, akaingia mtu dukani kapiga zake nguo za heshima, ana simu nzuri tu mkononi, halafu anamuuliza kijana wa pale, "Kutengeneza email shingapi?" Mie niko nahisi labda ni kama utani fulani, naona anajibiwa "elfu tano email ya kawaida, kumi na tano ya matumizi yote", mbaba wa watu akatoa kumi na tano. halafu anapokea simu na kuanza kuongea kwa misamiati, na misamiati yote hio hujui kufungua email?! Badilika.

2. Unalipia kuwekewe filamu/nyimbo kwenye laptop

Hawa wako wengi, unakuta mtu anachofahamu kwenye laptop ni kutumia Microsoft Word, Excel na PowerPoint. Mbali na hapo ni kubrowse mafile, kuplay muvi na miziki, kucopy na kupaste, basi. Haichukui hata dakika tano kujifunza kudownload audios au videos mwenyewe. Changamsheni ubongo.

3. Unasikiliza "The StoryBook" na kumeza kila kitu kama sahihi 100%

Hii nimekutana nayo na wanawake na wanaume wa umri 40+. Yaani mtu anakaa ananielezea jinsi Michael Jackson alivyouwawa kisa ni Illuminati sijui, au sijui siri ganigani na yuko serious. Muda wote unakua unajitahidi kubana kicheko usije kuwa fired. Kutafuta facts ni muhimu pia. Ukisikia kitu, fanya research ujiridhishe sio kumeza kisa kimeelezewa vizuri kwenye TV.

4. Unaendeshwa kirahisi na 'Watu wa Mungu'

Sikuhizi huko mtaani kuna manabii na mitume kibao, na wana brainwash watu wengi. Inatia huruma na kutisha kidogo kukuta umesoma na bado unaweza kuwa manipulated kirahisi hivyo.

Kwa mambo yanavyoelekea taratibu, dini ndiyo inageuka kuwa aina mpya ya imani potofu. Mchungaji akitaka gari mnamchangia, akitaka nyumba mnamjengea, akiugua anatulia kwanza apone, wewe ukitaka gari, unaenda kumpelekea sadaka ya shukrani akuombee. Unaweka mipango yako sawa, lakini kabla ya kuexecute unaenda sikiliza nabii anasemaje. Hii inatisha.

Nb. Naamini Mungu yupo, na ni muumini mzuri tu. Ila mambo mengine ni ujinga. Yaani mtu na suti yako, kazini uko mkali kwa wafanyakazi wengine halafu Jumapili unaenda kukanyaga mafuta. Badilika.

5. Unaogopa kukiri kuwa hujui kitu fulani

Kuwa na cheti, degree au PhD haimaanishi kuwa basi wewe una akili. Labda una akili, lakini haimaanishi unafahamu kila kitu. Nimekutana watu wengi wengi wanaogopa kukiri, kuwa hawafahamu kitu fulani, au wanaoogopa kuomba msaada wa kawaida kisa ya elimu au wadhifa walio nao. Hii inamaanisha unabaki kwenye sintofahamu milele.


6. Una dharau mtu uliyemzidi elimu

Kuna kitu cha mtu aliyemaliza kidato cha nne kujiona ni superior kwa wenye elimu ya la saba. Au mhitimu wa chuo, kujichanganya na wa kidato cha nne anaona kama haileti maana, kitu ambacho sio kabisa. Wanasema kila mtu unayekutana nae, iwe ni barabarani, msikitni, kanisani au kwenye daladala, ana maisha ameishi toka kazaliwa mpaka pale mlipokutana. Hivyo lazima kuna mambo kibao atakuwa anafahamu ambayo hufahamu na unaweza usifahamu.

Muhesimu kwa hilo peke yake.

Yapo mengine mengi, kwa kifupi tubadilike.

✍ Hizi tender za Sensa zimetoka watu wanaandikiwa application kwenye stationary.

✍ Mtu anaomba kazi hajui andika proposal au kupangilia wasivu wake.

✍ Kujielezea kwa Kingereza walau dakika 5, hata kwenye maandishi ni shughuli.

✍ Unapendelea filamu zilizotafsiriwa halafu hata huyo VJ akikudanganya hata haugundui na subtitle zinaonesha!

Badilikeni, mnatia aibu.
 
2012 wakati na-apply chuo mimi na jamaa yangu tuligoma kabisa kufanyiwa applications za mkopo na chuo.

Tulifanya wenyewe mwanzo mwisho, na enzi hizo hamna simu janja wala nini. Ilikuwa mnaenda internet cafe mnalipia elfu 2 lisaa, halafu unakuta websites za HESLB & TCU full kusumbua, mnaweza kwenda kushinda siku nzima na msifanikiwe hata kufungua sites😂

Nashangaa sana kizazi cha sasa kina kila kitu lkn kiko very lazy kwenye kujifanyia vitu wenyewe.😡
 
5 & 6 muhimu kuzingatia.

1, 2 & 3 inategemea na muda. Si lazima nifanye kila kitu.

4 watakuja wenyewe watujibu. But without God, you're nothing. Usisahau.
I'm a believer mkuu. Lakini mambo mengine sasa yamegeuka wizi wa mchana kweupe kwa jina la Mungu.
 
Unaweza kuwa na degree ukashindwa kuelewa Elimu ya Mungu. Msingi mkubwa wa kuelewa Elimu ya Mungu ni kuamini. Kama huwezi kuamini basi unakua umeshafeli elimu ya Mungu.
Mafundisho ya hiyo elimu ya kiMungu sipingi. Ila siku hizi karibia kila kitu kinahusiana sadaka.
 
Nasikitika kusema kwamba na wewe ni mmojawapo wa hao uliowataja hapo juu.

Kama wewe ni msomi ambae hata kuandika lugha yako ya taifa inakushinda basi Taifa lina hali ngumu sana. Mhumini ndo kitu gani? Waswahili wanasema nyani haoni kundule.

Kabla ya kutoa kibanzi kwa mwenzako toa kwanza kwako.
 
Wengi hasa ktk masuala ya TEHAMA husingizia wapo busy kumbe hata hawajui.Na unakuta ni ishu ndogo kabisa,ila zaidi naona wazee wa miaka 40 na kuendelea ndo wanasumbua sana ktk nyanja hiyo!
 
Wewe pia badilika.Hapo kwenye masuala ya tehama laumu CCM,sio wasomi unaowataja.

Angalia mfumo wa elimu somo la tehama MTU anakutana nalo chuo,tena hapo atasoma semester mbili Tu unategema awe competent?

Wewe iamboe CCM somo la tehama lifundishwe kuanzia nursery uone Nani ataomba kusaidia kwenye simu/computer
 
Nasikitika kusema kwamba na wewe ni mmojawapo wa hao uliowataja hapo juu.

Kama wewe ni msomi ambae hata kuandika lugha yako ya taifa inakushinda basi Taifa lina hali ngumu sana.
Mhumini ndo kitu gani? Waswahili wanasema nyani haoni kundule.

Kabla ya kutoa kibanzi kwa mwenzako toa kwanza kwako.
Duh , mie sio msomi, mkuu Pili hakuna mahala nimeandika kukosea spellings ni tatizo. Asante.
 
Back
Top Bottom