Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Miaka ya 60 alikuwepo mtangazaji maarufu jina lake Kwege Munthali, mtangazaji huyu alijipatia sifa sana kutokana na umahili anapokuwa studio kama ambavyo wenzake nao walijipatia sifa za aina hiyo tofauti na hawa tulionao sasa.
Bahati mbaya yeye na wenzake walifariki mtaa wa Shaurimoyo Ilala Dar es Salaam wakati wakivuka reli, hamadi! treni hiyo, ikalikumba gari lao na kusababisha vifo kwa watangazaji hao vijana, lakini yeye na wenzake majina yao yaliendelea kusikika TBC kwa muda mrefu japo hawakuwepo! Kwege Munthali aliacha mke na familia.
Kesho Ijumaa tarehe 4 October adhuhuri mke wake Kwege atazikwa Kinondoni kwenye makaburi ya zamani mahali alipozikwa mume wake.
Taarifa hii natumai itawafikia ndugu, jamaa na marafiki wa Kwege na mke wake.
Bwana alitoa na sasa Bwana ametwaa, ameni.