Kwa wastaafu wa TBC waliokuwepo kazini miaka ya 60 na waliokuwa wapenzi wa kusikiliza TBC miaka ya 60, tanzia hii huenda inawahusu

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
21,741
Reaction score
26,735
Miaka ya 60 alikuwepo mtangazaji maarufu jina lake Kwege Munthali, mtangazaji huyu alijipatia sifa sana kutokana na umahili anapokuwa studio kama ambavyo wenzake nao walijipatia sifa za aina hiyo tofauti na hawa tulionao sasa.

Bahati mbaya yeye na wenzake walifariki mtaa wa Shaurimoyo Ilala Dar es Salaam wakati wakivuka reli, hamadi! treni hiyo, ikalikumba gari lao na kusababisha vifo kwa watangazaji hao vijana, lakini yeye na wenzake majina yao yaliendelea kusikika TBC kwa muda mrefu japo hawakuwepo! Kwege Munthali aliacha mke na familia.

Kesho Ijumaa tarehe 4 October adhuhuri mke wake Kwege atazikwa Kinondoni kwenye makaburi ya zamani mahali alipozikwa mume wake.

Taarifa hii natumai itawafikia ndugu, jamaa na marafiki wa Kwege na mke wake.

Bwana alitoa na sasa Bwana ametwaa, ameni.
 
Ila TBC kuna wazee knoma, niliwahi kupata nafasi ya kuona baadhi ya wapiga picha wao aisee 🙌 em waige kwa Azam TV pale kuna vijana hadi wengine unaweza kudhani ni watoto na kazi kila mtu anaiona.
Unakuta mtu ana miaka 50 yupo anahangaika na camera 🗑️
 
May all beings attain enlightenment.
 
= umahiri

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
= umahiri

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
= umahiri

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…