Uko serious kweli na hilo tatizo?
Kama ndio mbona umetoa maelezo yasiyojitosheleza?Ww mwenyewe umesema unahisi tatizo kma ukungu sasa na sisi unataka tuhisi huohuo ukungu?? Maelezo ya kwenye maduka ya oembejeo ni kama hanachanganya mbona hujasema wamekwambia sjida inaweza kuwa nn?
Be seriois km ww ni mkulima eleza tatizo likoje,piga picha jani la mmea lionekane vizuri ndipo unaweza pata msaada stahiki.
Kama ndo unataka tuuhisi huo ukungu basi utakuwa wenyewe piga dawa yoyote ya ukungu.
Nina njia mbili ambazo hutumii madawa.
Njia ya kwanza.
Kama sio eneo kubwa fanya hivi. Chukua vitunguu swaumu viwili vikubwa maji lita mbili kijiko cha chai cha mafuta ya kupikia na kijiko cha chai sabuni ya kuoshea vyombo au mikono.. Menya vitunguu swaumu twanga weka jikoni kwa dakika 10 na maji lita 2. Chuja. Chukua sabuni na mafuta changanya. Halafu miminia kwenye maji uliyochuja. Chukua spray ya kupigia dawa. Weka piga kila.baada ya siku 3 baada ya siku saba mimea itakuwa iko vizuri.
Njia ya pili
Kama una maji yenye presha kali safisha hiyo mimea hakikisha unasafisha mpaka nyuma ya majani. Hii ni nzuri kwa mimea mikubwa. Baada ya kusafisha ikiwa bado ina maji tupia jivu kidogo.