MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Ninaandika hili kwa uchungu mwingi sana. Kumekuwa na matukio mengi hapa nchini ya watu kujeruhiwa au kuliwa kabisa na fisi. Na mara nyingi wahanga huwa ni watoto hasa wale wenye umri mdogo. Hili jambo linalotia uchungu mwingi mno. Mkoani Shinyanga ndo kumekuwa na matukio mengi ya fisi kuleta madhara kwa binadamu. Matukio ni mengi mno yaliyoripotiwa.
Sasa hivi mkoa wa Arusha hasa wilayani Karatu kumeibuka mfululizo wa matukio ya fisi kula watoto. Huko kata ya Endabash fisi wameripotiwa kusababisha vifo vingi ndani ya muda mfupi. Kijiji cha Basodowish kimekuwa na wahanga wengi. Ninavyoandika tayari jana huko kwenye kata ya Eyasi kuna mtoto wa miaka mitatu nae kaliwa na fisi. Yalipatikana mabaki yake machache mno ndo yakazikwa. Ni habari zinazohuzunisha sana.
Mimi kama msomi niliamua kuuliza kama idara ya wanyamapori imechukua hatua yoyote kufuatia matukio haya nikajibiwa walichosema ni kutoa tu pole na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari. Sikuridhishwa kabisa na haya majibu kwasababu idara imejaa wataalamu wanaotakiwa watoe majibu ya kitaalamu na kuchukua hatua za kitaalamu ili kuepusha uhasama baina ya binadamu na wanyama. Hakuna haja ya kuwa na watu wanaojiita wataalamu wa wanyamapori huku wananchi wakiendelea kuzika wapendwa wao kwa vifo vinavyotokana na wanyama.
Idara isiwe inajikita zaidi kujali wanyama kuliko binadamu wenzao. Kuna tetesi zinasema kwamba kumekuwa na uhamishaji wa fisi toka kreta kwenda vijiji jirani ili kunusuru wanyama walioko hatarini kupotea huko mbugani. Kama ni kweli basi hii idara itakuwa imekosa ubinadamu kwa 100%. Kwa asilimia kubwa naweza nikaamini hizi tetesi kwasababu pamoja na wilaya ya Karatu kupakana na Ngorongoro hakukuwapo na matukio ya watu kuliwa na fisi. Haya mambo yameanza kutokea hivi karibuni.
Idara ya wanyamapori chukueni hatua vinginevyo mtakuwa mnamhujumu Mama Samia na serikali yake. Watu wa haki za binadamu nanyi nimewashangaa sana kwa ukimya wenu. Huwa mnatetea haki za binadamu au haki za CHAMA CHA MBOWE? Mbunge wa Karatu kama unasoma hapa jua kabisa 2025 utapata tabu sana hili jambo lisilopfuatiliwa. Mbunge wa viti maalum Cecilia Paresso kupitia CHADEMA nawe pia umekaa kimya kama vile halikuhusu.