Kwa watu wa mkoa wa Mara


Bila kumsahau Lieutenant General Mwana Mtoka Pabaya wa Wilaya ya Serengeti, Tarafa ya Ngoreme, Kata ya Kisaka, Kijiji cha Nyibhoko.

Ujasiri wetu uliishia katika kuwasaidia WAHAYA wasiendelee kuolewa na Iddi Amini Dadaa
 
Kwanini unasema umekaa kikabila?,tusaidiane ili turekebishe,Mara ni yetu yego.

Mkuu kitu cha kwanza ambacho naweza kushauri ni kuwa watu kutoka mkoa huo wapungue kwenye idara ambazo utendaji wake unategemea watu mechanic, yaani idara ambazo in nature ni brutal. Kama vile polisi, jeshi and alike. Kidogo hizi idara zinaleta sifa mbaya kwa mkoa na watu wake...jaribu kuangalia watu wa mkoa wenu katika vyombo vya usalama unaweza kusikitika. Sijui labda nyie wenyewe mnapenda.
 
Nakushukuru kwa ufafanuzi mzuri,mimi ni mongoreme kama nilivyjitambulisha,kama utakumbuka vema kuna bwana mmoja aliwahi kuwa mbuge wa serenget miaka 90,bwana Maro George(Mwita) ni mongoreme,hakuwa mtu mwema,aliposhindwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2000,aliungana kwa siri na mgombea wa CUF bwana John Mosena Nyambabe kumpigia kampeni huku akipiga nyimbo za kuchochea chuki kati ya wangoreme na wairege.Hii akiri ya kufikiria madaraka bila kujali mustakabali wa wilaya na mkoa ni hatari sana na watu kama hawa hatutakiwi kuwaunga mkono hata kidogo.Kama sasa Wahutu na Watutsi wameungana na wanafanya mambo ya maendeleo,sisi tunaweza sana.Kuhusu Luge ni kweli kabisa ulichokisema,hata wangoreme hawamwamini,alinufaika sana na vurugu.Watu wa namna hii hatuwahitaji kabisa.Nilishafika Mbalibali mara nyingi na nina marafiki huko.
 
Mimi nafikiri mtoa mada ana lengo zuri sana na kwa kweli ameeleweka. Kimsingi ni kuanza mikakati ya jinsi ya kuanzisha huu umoja.
Mimi niko Rorya - Mara na niko tayari kuunga mkono juhudi zote za kujenga na kuimarisha umoja huu.
Cha msingi ni kuachana na lawama na tuanze mshikamano kuanzia hapa tulipo kwa lengo la kusonga mbele na si vinginevyo! Ahsanteni sana, tuko pamoja!
 
Salute,
Big up kwa muanzisha mada na wachangiaji wote.
Enye Mzanaki, yika ni Busegwe mission harya wa Kohi, mzukuru WA Mtarima.

Katika msfara WA Mamba na Kenge wamo. Nasema hivyo maana tayari tumekubali weakness zetu ziendelee kutumaliza wenyewe kama wachangiaji walipita tena cha ajabu Wana iponda idea na kujitambulisha wao ni WA Mara pia...jamani are these guys seriouse? Yaan inamaana mpaka sasa hawaoni umuhimu WA kufanya mabadiliko?

Mi Sita taja majina wala kuwanyooshea vidole wale wote wazazi wetu waliotoka mkoa WA mara na kushindwa kukumbuka kwao na ndo hasa tatizo kubwa of which sisi sasa ambao tumeliona (si ajabu wao hawakuliona hahaha) inabidi tufanye hima na kuleta mabadiliko...inawezekana kabisa!! Tuweke UJINGA wetu pembeni ili iwezekane.

Saganka? We nambie whatz next ili tulianzishe, nakuunga Mkono na tuko pamoja japo nimeona umeisha aanzisha katiba na uko mbioni kuisajiri. Can u share pls?

Uzuri mwingine ni kwamba sasa Wana JF tuta anza kufahamiana uso kwa uso hahaha na nadhani hili halikwepeki iwapo tutataka kuleta mabadiliko ya kweli kwa mkoa wetu.

Hatujachelewa!!!


founder and CEO of www.oric.co.tz and www.aio.co.tz skype: alfred.kohi, 0784800989, 0715800989/0715800989
 

Jambo moja linalonikera sana ambalo bado nalitafutia njia muafaka ya kuli address ni kitendo cha TANAPA kuweka makao makuu ya mbuga ya serengeti (SERENGETI NATIONAL PARK-SENAPA) mkoani Arusha. Hii ni dharau kubwa sana kwa wanaSerengeti lakini ajabu ni kwamba hakuna kiongozi yeyote anayeliona hili na kulipigia kelele.

Ndugu zangu wana Mara pamoja na mambo mengine, ni lazima tuishinikize serikali itupe haki yetu ya makao makuu ya mbuga ya serengeti kuwepo mkoani kwetu, wilayani kwetu mjini Mugumu.

Nimebahatika kufikka katika baadhi ya hifadhi/mbuga zetu zilizopo hapa nchini kama Mikumi, Manyara, Ngorongoro, Udzungwa, Ruaha, Kitulo, Saadani, Mkomazi, Tarangire huko kote makao makuu ya watendaji/ofisi za mbuga/hifadhi hizo ziko katika mbuga/hifadhi husika, kwanini sisi ya kwetu Serengeti iwekwe Arusha? kwa maslahi ya nani?
 
Akohi nimekupata vema,ni kweli nina draft ya katiba hapa,nita-share na kila anaetaka.Kuendelea kuzungumza huku tumejificha nyuma ya keybord ni dalili za kushindwa hata kuliko wazazi wetu.Namba zako nimeziona,nitakutafuta baadae kidogo.Nafanya kila lililo ndani ya uwezo wangu ili katiba ipate usajiri,nitaitangaza ili kuungwa mkono,na hapo tutafahamiana sana tu.Mara ni yetu, tuna rasilimali za kutosha,tunahitaji kuijenga.
 
Binafsi origin yng sio mkoa wa mara ila nimeishi hko kwa muda mrefu sana na hasa wilaya ya serenget.Ukweli ni kwmba raia wa hko ni wachapa kazi sana hasa kilimo na ufugaji,nani asiyejua kuwa mkoa mzima na hta kanda ya ziwa wanategemea sana zao la mahindi,ulezi,mtama na mihogo kutoka wilaya ya serengeti na tarime! Tatizo kubwa la wananchi wa maeneo hayo ni kutolipa kipaumbele suala la elimu kwa muda mrefu japokuwa sasa hivi naona wameamka kwa kiasi kikubwa hasa baada ya kudhibitiwa kwa suala uwindaji wa wanayama pori, vijana wengi wa wilaya ya tarime,serenget na bunda walikuwa wamekalia uwindaji tu kama chanzo cha kupata fedha na kununua mifugo mfano vijiji vya machochwe,kisangura,bwitengi,miseke,kebosongo,koleli,natta,issenye,rwamchanga n.k ilikuwa ni full kuwinda kitu ambacho kwa sasa ni ADHIMU KWAO. Ili kutumia fursa zilizopo elimu ni muhimu sana kwa mfano SINGITA LODGE (VIP,GURUMET FUND) ajira zilikuwa nyingi sana na kila kijana kijiweni alikuwa nawaza kufanya kazi huko pamoja na kupewa kipaumbele bado ajira hizo zilijaa watu kutoka daa,arusha,moshi,mwanza n.k kwa sababu vijana wengi hsa wa serengeti walikosa sifa stahiki (hotel,tourism,wild life management skills).Amin usiamin nimeshuhudia matangazo yakipelekwa hko vijijin mara kwa mara na hata kurudiwa ili mradi tu wananchi kuzunguka maeneo yale wapatikane bado ilikuwa ni ngumu kuwapata wenye sifa.
Ukienda pale hotelini utakuta zaidi ya asilimia 85% ya wafanyakazi ni wa mikoa mingine,wana mara wengi wameajiriwa kma ant-poachers (wenye kutumia nguvu kufukuzana na majangiri porini) tena approach waliotumia wale jamaa wakati wa ajira za ant-poachers ni kutafuta wale waliokuwa majangiri/wawindaji sugu na kuwapa mafunzo ya kijeshi kisha kuwaajiri ndio maana wamefanikiwa sana kudhibiti sana uwindaji maana wale jamaa wanajua njia na mapito ya wawindaji wote.NAAMINI WANAMARA MKIAMKA KIELIMU MTAFANIKIW SANA MAANA U ARE HARD WORKERS NA KUNA FURSA NYINGI SANA ZA KIUCHUMI HASA HIFADHI YA SERENGETI NA MADINI.I wll join u mkianzisha umoja ambao unasound na sio uliokaa kisiasa siasa.MSIISHIE KULALAMIKA JITAYARISHEN KUGRASP FURSA KWA KUWA NA SIFA STAHIKI.good time mara peoples.
 

Dr. Mwita namfahamu sana, those days akiwa mbunge alikuwa akinipa lift mara moja moja nikienda shule Moshi. Na hata hivyo mzee wangu alikuwa akimuuunga mkono sana hata kampeni zake za ubunge zilirahisishwa sana kwa kitendo cha wakurya kumuunga mkono kwa wingi sana lakini mambo aliyowafanyia baadhi ya ndugu zetu imebaki historia. Kuna baadhi ya watu alichukua watoto wao wa kike kwamba anakwenda kuwasomesha lakini alichowafanyia ni wao wenyewe wanajua.

Sasa tuliposikia kwamba baadae alianzisha siasa chafu za ukabila dhidi ya Nyambabe kwakweli watu walimshangaa sana na hali hiyo imerudisha nyuma sana hali ya maelewano iliyokuwa imeanza kujengeka miongoni mwa wangoreme na wakurya. Tunatakiwa tupambane sana na wanasiasa wanaohubiri siasa za chuki kwakuwa wataturudisha nyuma sana ambako hatuhitaji kurudi huko tena.

Btw, nina rafiki zangu wangoreme wengi tu na nikiwa nao najiona niko na brothers wa damu kabisa. Kwahiyo katika hili tuko pamoja sana.
 
Hata uwanja wa ndege wa Mugumu umekuwa hadithi,Tunatangazaje Mugumu kama kitovu cha utalii Mara bila miundombinu bora,hasa usafiri.
 

Kwakweri inakera sana, mambo sio mazom kabisaa! inabidi juhudi zichukuriwe!!!!!
 
Hata uwanja wa ndege wa Mugumu umekuwa hadithi,Tunatangazaje Mugumu kama kitovu cha utalii Mara bila miundombinu bora,hasa usafiri.


Nimesikia Mmarekani Tudor Jones amejitolea kutoa fedha za ujenzi bado serikali ndiyo haijatoa kwa upande wake ili shughuli za ujenzi zianze kitu ambacho kimemfanya mmarekani huyo kutaka asimamie mwenyewe ujenzi kwa kutafuta mkandarasi. Nadhani bado serikali inakuna kichwa kwakuwa mmarekani yuko tayari ispokuwa wao ndio bado wanasuasua.

Vile vile tunahitaji miundombinu bora ya barabara kutoka mugumu kwenda mbugani, kutoka mugumu kwenda bunda, kutoka mugumu kwenda tarime na kutoka mugumu kwenda maeneo mengine yanayotuzunguka ili tuweze kunufaika na shughuli za utalii na kiuchumi.
 
Wewe umefanya nini mkuu au unalalamika tu, mimi binafsi sipendi watu wanaolalamika tu bila action plan.Ni kweli pana tatizo. Bunda ndo wilaya kwanza kwa umaskini, sasa chukua hatua tuanzie hapo mkuu
Mihayo,kwa kuanza tayari nime-draft katiba ya Muungano wa Vijana wa Serengeti,naomba tuungani kuiokoa Mara yetu.
 

Naamini si kweli kwamba kuna ukabila,
Tatizo la mara nafikiri ni lile lile la mikoa mingi Tanzania, tatizo lake namba moja ni
1. Elimu, wakazi hawakwenda shule na walioenda ni wachache sana, tulikalia kuvua jiswi yani chengu, sato,gogogo, jinembe, furu, kamongo nk. wakati wengine wamekalia mifugo. Na kupigana na masai kwa kutumia mishale na kuibiana ng'ombe.
Na kama shule basi nikizazi kuanzia miaka 70-80 ndo kimegutuka.

2. Imani za kishirikina kama ilivyo kigoma, subawanga nk, hata hivyo hii point imefungamana zaidi na namba 1 juu. Hii imani inatisha wengi sana na wengi wanatimua wakijiona kama wana elimu ama mali, ni imani za kutisha hizi za kishirikina ndo zinarudisha maendeleo nyuma. Kule watakutisha kwa mamba zao na viboko vyao integrated with ungo. Maendeleo yatapatikana kweli?
Tusilaume bure watu wengine, mtu anayekuletea barabara ya rami anakutakia heri, acheni kujidanganya. waingereza wenyewe mbona wamepitisha daraja tunnel ndani ya maji hadi ufaransa, sweden mbona wamepitisha barabara juu ya maji hadi norway, na bado hatujalalamika wanawabugudhi samaki? gutukeni.
 
Na kutoka Mugumu kwenda Musoma mjini kupitia Kebancha,Daraja Mbili,Kenyana,Ring'wani Masinki,Sirori Simba,barabara hovyo hovyo.
 

Maelezo yako na ushauri wako nakubaliana nao kwa kiasi kikubwa.
Isipokuwa nilitaka nikufahamishe jambo moja kwamba wakazi wa serengeti kwa asili shughuli zao kubwa ni ufugaji, kilimo na uwindaji, wamekuwa wakifanya uwindaji huo miaka na miaka lakini bado hawakuvuruga ecosystem kama ambavyo tumekuwa tukilazimishwa kuamini. Wananchi wa serengeti hawajawahi kutegemea uwindaji kama njia kuu ya kujipatia kipato ama maendeleo bali kilimo na ufugaji.

Suala la vijana kukaa kijiweni lilikuwepo na bado lipo kutoakana na kutokuwa na mwamko wa elimu, ingawa sasa mambo ni tofauti sana, vijana wengi sana sasa wanasoma na hao ndio mategemeo makubwa kwa ajili ya maendeleo ya wilaya yetu.

Nikizungumzia ajira za Mahotelini sio kweli sana kama unavyodai, tunao vijana ambao si wengi waliokuwa wamesomea kozi za hoteli na utalii lakini bado hawakupata ajira katika mahoteli yaliyoanzishwa, hii ilisababishwa na mameneja waajiri wengi kuajiri watu wao ama watu kutoka huko kwao, kiujumla kulikuwa na upendeleo mkubwa sana. Mimi binafsi mdogo wangu alikuwa amemaliza certificate ya hotel management lakini alifanya intervie mara tatu na kuachwa, alipokuja dar akafanikiwa kupata kazi hotel moja hapa jijini. Baada ya wananchi kulalamika kwamba watoto wao hawaajiriwi na badala yake wanaajiriwa watu wengine hasa kutoka Arusha, Kilimanjaro, Mwanza na Kenya ndipo baadhi ya waliokuwa na sifa wakapata nafsi ya kuajiriwa na mdogo wangu wakamuita na kwakuwa walimpa maslahi mazuri comapred na huku alikokuwa nikamshauri aende.

Lakini pamoja na hayo yote niliyosema bado tunawajibika kupigana zaidi ili kufikia malengo kama mikoa na wilaya nyingine.
 
Kisayansi samaki wanapenda sana sauti zenye/zisizo na mpangilio maalum,lakini wanyama hawapendi.Madereva wetu pamoja na kwamba lami haijawekwa wanagonga wanyama,itakuaje ikiwekwa.Anyway kama hilo si sehemu ya tatizo itajulikana tu.
 
Mimi sio Mkurya lakini nimekaa ukuryani kwa miaka 6 sasa katika kutafuta,hakuna wilaya yoyote ya mkoa wa Mara sijawahi kufika, anzia Serengeti - Mugumu kupitia Nata, Mgeta mpaka Bunda, pitia Nyamswa, Butiama, Kyabakari mpaka Musoma,katisha pale zero kwenda mkoa mpya wa kipolisi wa Tarime, Rorya mpaka Silari kwenda mpaka majita hadi Ukrerewe, from my heart nakuambieni hata mtengeneze muungano wa vijana, wazee, watoto, wanawake na hata watoto ambao wametungwa mimba HAMTAWEZA kufanikiwa. Naesema hivo kwa sababu system imewafanya nyie mnyamaze msiweze kusema chochote, sasa unategemea kila kona ya serikali wameweka watu wa Mara nani ataweza kukohoa wakati anakulazake 10% na anataka kupata heshima serikalini.

Mfano ifuatayo inaonesha kuwa vijana wa mkoa wa Mara mtakufa maskini hata kama mna fursa nyingi sana

-Ukiingia kwenye mbuga ya Serengeti na hoteli zake 70% ya wafanyakazi hata zile kazi ndogondogo za kuosha vyombo wanatokea Arusha na Mwanza hapo inatakiwa muamke mseme inatosha,pelekeni vijana wakasomee mambo ya utalii vyuoni
- Nduguzanguni Wanata, Waikoma na Wanyichoka nyie ni bure kabisa mpo karibia na mwekezaji wa Singita Grumeti Reserves lakini kazi yenu ni kulalama tu na ajira wanachukua vijana wa mbali, kisa hamjaweka mkakati mathubuti wa kuajiriwa pale manachojua ni kwenda kuomba tumisaada twa kijinga eti mfundishwe kurina asali upuuzi mtupu
-Machimbo ya dhahabu yapo kwenu lakini waajiriwa wanatokea mali sana kisa hamna makakati wa kimaono ndio maana hata hizo sehemu za wachimbaji wadogowadogo wameamua kuwanyanganya na hamtafanya lolote milele daima maana nyie vijana wa Mara mumejaa ukabila mara utaskia yule ni mjaluo, yule ni Mtana yule ni mwisenye mara yule ni muikizu yaani bure kabisa
-Nimetembea duniani lakini sijawai kuona vijana waoga kama wa mkoa wa Mara, ukisikia Mkurya eti ni makali basi ni kwa makabila ya huko huko kwao lakini kwa kabila lolote linalotokea mkoa mwingine Mkurya anaweka mkia matakoni anamwachia anafanya anachokitaka
 

Ha ha haaa, mkuu hii ni kweli, na ungeanzia na Nyerere, kwani hakuchangia kuididimiza Mara? Iweje mapato mengi ya Serengeti yainufaishe Arusha? Ili suala kwa kweli huwa linaniuma sana, japo wengine wanadai hii inaonekana ni sera za majimbo ambazo ni za kibaguzi, mm nasema sera ikiyopo ni ya kipuuzi zaidi!
 
Duh! lugha kali sana hiyo.Lakini ujumbe umefika,lugha uliyotumia tutaitumia kama changamoto kuanzisha muungano huu.Asante sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…