Ni kweli, mimi pia mzaliwa wa huko tena hapo Mtaa wa Kawawa.Hali ya mkoa si nzuri kihistoria na kiuchumi. Hatuna sababu sana ya kujigawa kijimbo ili tufaidi rasili mali zetu ila kuna haja ya KUBADILIKA kitabia, sifa za kijinga pamoja na kukumbuka kurudi nyumbani.
Sio mpaka upate cheo ndio ukumbuke kurudi nyumbani kama Prof. Mhongo alivyofanya hivi karibuni. Kama wanavyofanya wana-diaspora huko ughaibuni basi kuna haja ya kuwahamasisha wana Mara kuwa na tabia ya kurudi nyumbani, kuwekeza, kujenga pamoja na kushiriki shughuli za maendeleo hata kama si kwa kupitia siasa.
Mimi binafsi nimewahi kuchangua ku-elimisha watoto wa huko home yaani kuwapiga shule.Nimepita na darasa langu la tuition hapo Mkendo Primary na hatimaye Mwalimu wa kawaida hapo Mwembeni Secondary.Huu kwangu ulikuwa mchango pia.
Tabia ya kukatalia Dar na kwinginepo na hatimaye kurudi tukiwa ndani ya sanduku kwa kweli ni fedheha. Tazama viongozi hao uliowataja hawakujenga kwao, hawajui maisha ya kwao na kila wakipita kikazi ni Hotelini na kukimbia mji kisa eti uchawi ama kukwepa kuombwa pesa na ndugu zao walio duni.
Wanafurahia sasa kuonekana wako juu,vyeo,pesa huku kutoa msaada ni kama mbingu na ardhi.Tuache tabia hizi wana MARA.