Kwa watu wa mkoa wa Mara

Tunabaguliwa natunabaguana jaribu kuangalia mabango ambayo yapo kwenye mpaka wa Mara/mwanza sasa Simiyu BANGO la Kutokea Mara kuingia Mwanza linasomeka hivi; KARIBU MKOA WA MWANZA na kisha angalia bango la kutokea mwanza kuingia Mara linasomeka hivi ; SASA UNAINGIA MKOA WA MARA as if kuna tahadhari unatakiwa kuwa nayo unapokuwa mara huu ni ubaguzi mkubwa sana tunaofanyiwa wana mara wote uwe mwana siasa ama not unabaguliwa hivyo
 
Na Mie nipo mbele yenu kwa 100%. Imagine mji kama bunda next to national park haina hata hotel za maana. Watalii wanarudi arusha wote. Kwetu karukukere ndo kama zizi la ng'ombe
 



Hapo kwenye red, inanishangaza sana kwani yule mzungu "PAUL" akija na timu yake wanaua wanyama ovyo mamia kwa mamia, wanaondoka na ngozi na vichwa tu. Sisi wakazi wa hapo tukigusa hata sungura unapigwa risasi. Jamaa hawa wana hela sana hata mkuu wa nchi analijua hili. Hoteli yao ndiyo imeshika namba moja kwa ubora duniani.


hapo kwenye nyeusi, ile hoteli ni kweli ni ya mkuu wa kaya inaitwa BILILA
 

0687315600, mkuu tutafutane tuijenge Mara yetu
 

Pole ndugu yangu Saganka haya mambo yatawezekana tu kwa kuunda serikali za majimbo mie nikiteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Mara nitakuwa na uchungu gani na huo mkoa iwapo kwetu ni Dodoma? Pili iwapo nitakuwa nimetoka Dodoma ambapko hakuna miti kwa wingi kama Mara nikifika Mara sintakuwa na uwezo wa kujua kama Mara ilikuwa na misitu mingi kabla sijawa mkuu wa mkoa wa mara mie nitaona tayari ina misitu kwa kulinganisha na nilikotoka yaani Dodoma kumbe ni tofauti iwapo Mwita Maranya au Chacha Wankuru Mwita angekuwa ni gavana wa Mara maana yeye anajua historia ya Mara atalingamisha Mara ya sasa na ya miaka ya 80 na kujua kwa sasa Jangwa linanyemelea Mara kwa kifupi anapakulingalisha na alipokuwa anakua lakini mie niliyetoka Dodoma sina pa kulinganisha, sina uchungu na Mara na pia naweza uza ardhi kwa wageni na kutajirika haraka kwa kujenga kwetu wala msijue maana hakuna ajuaye nitokako tofauti na Mwita Maranya au Chacha Wankuru Mwita akitajirika ghafla mtahoji maana mnajua historia yake na wazazi wake na alipokulia.
 
Viongozi wanaotoka ni wabinafsi hivyo wanajijali wao na kuwaacha wana Mara hohehahe. But tutalalamika mpaka lini we need to woke up and move. Ni leo sio keshona tuachane na siasa
 
Ndugu yangu hawa vijana wa mkoa huu na VIMORO HASA WALIOKO PEMBENI MWA HIFADHI NI VIGUMU SANA KUSAHAU HICHO " IBING'ARA, ANYAMA ORI " Ha ha ha ha ha ha very great power is needed to change them ila tutie nguvu ili tuwatoe kwenye fikra hzo maana ni watanzania wenzetu.

Mm nimekulia huko na kusoma primary na o level huko yaan tulifaulu wengi tu wakati wa kuhitimu elimu ya msingi ila tuliojiunga sec ni kiduchu na hasa wa kutoka mikoa mingine,wengi wao walisema kusomesha mtoto 4 yrs n kupoteza muda wa uzalishaji mali na watoto wao nao walikuwa wanashabikia tu wanashabikia hilo hadi namaliza chuo kikuu pale mliman kulikuwa na vijana kama 4 niliowafahamu kutoka serengeti hii ni aibu AMKEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEENI SASA TUTAWAUNGA MKONO SISI WAKUJA HUKO.
 
Mgawanyiko upo hata ndani ya vijana wenyewe; pale chuo kikuu cha mlimani (UDSM) nakumbuka kulikua na vyama vitatu vya mkoa wa Mara: kimoja kinajumuisha makabila yote yanahusiana na jamii ya wakurya, kingine makabila yanayohusiana na jamii ya wajita, na kingine kabila la wajaluo! Ukiangalia hata chaguzi zote Musoma mjini nasikia kampeni huwa zinaendana na makundi hayo matatu ya kikabila.
Ingawa ni kweli kuna umuhimu wa kuangalia maendeleo ya mkoa na kuachana na mambo ya migawanyiko iliyoko isiyokua na maana yoyote.
 
Nilikuwa Mugumu, sasa hivi watu wa mikoa mingine ndio wanakuja kuwekeza ili kutumia opportunities zilizopo na wenyeji wamekalia kubaguana, majungu na fitina miongoni mwao.
 

Sio wajita tu,hata ukifika serengeti utakuta kura zinapigwa kiukabila.Kuna haya makabila yanayojiona giants(Wakurya na Wangoreme),wanawaacha waikoma,wanata na waisenye kuwa watu wa kuunga mkono tu upande mojawapo.Tuondoke katika fikra hizo,maana tumekuwa tukikosa viongozi wa maana kwa ushabiki tu.Kuna bwana mmoja ni Mwisenye,anaitwa Daniel Mhochi,ni mtu wa maono kweli,lakini amesaka ubunge tangu mwaka 90 hadi 2010 hakupata kutokana na yeye kutoka katika kabila lenye watu wachache.Hayo ndo baadhi ya mambo ya kuondokana nayo.Najua itachukua muda,lakini tunaweza.
 
Mimi pia mjita, jamaa amekariri sifa za kijinga mara nyingi hadi post limepoteza ladha, halafu hana solution hata moja yeye ni wa kulalama tu, wacha niende jukwaa la mahusiano........

Nakutakia kila la heri katika jukwaa la mahusiano.Lakini ingekuwa vema kama ungepata muda wa kusoma na kuelewa.Lakini pia kujua tatizo ni hatua nzuri sana.Zaidi ya yote nimesema kuwa tayari nina draft ya katiba ya Muungano wa Vijana,ni hatua nzuri kwangu mimi.Hata hivyo kukosoa ni sehemu ya maendeleo.
 
Mihayo,kwa kuanza tayari nime-draft katiba ya Muungano wa Vijana wa Serengeti,naomba tuungani kuiokoa Mara yetu.

Nilifikiri ni katiba ya Mkoa wa Mara kumbe ni Serengeti pekee!:A S cry:
 
Nilifikiri ni katiba ya Mkoa wa Mara kumbe ni Serengeti pekee!:A S cry:
Samahani ni makosa tu madogo,ni draft ya Muungano wa Vijana wa Mara(MUVIMA).Utanisamehe wakupita.
 

Kwahiyo wewe unafurahia wazungu kuja kuwinda wanyama wetu kwa raha mustarehe lakini sisi wenyeji ambao tumekulia mazingira hayo miaka na miaka tunanyanyaswa tusiguse nyama pori kabisa.

Siku za nyuma kulikuwa na msimu wa uwindaji, mara moja kwa mwaka, ambapo uliwekwa utaratibu wa kutoa vibali vya uwindaji kwa wananchi. Hapo ndipo wananchi wanaoishi kuizunguka mbuga ya serengeti walipata nafasi ya kuuziwa nyama pori kutoka kwa wawindaji walioruhusiwa kufanya biashara ya uwindaji wa nyama pori. Kwa sisi tuliozaliwa na kukulia Serengeti huwezi kututenga kitu kinachoitwa nyama pori, iwe mbichi ama iliyokaushwa. Hilo halikuhitaji kuwa na degree kulitambua, ni common sense tu.

Kwamba hushangai wamasai kuachwa kuendelea kuishi ndani ya ngorongoro lakini unashangaa wakurya na waikoma kula kimoro/king'ara? Kuna vitu vingine unapovifanya ambavyo vina athari ya moja kwa moja na maisha ya watu lazima uwape kitu mbadala, si suala la kukurupuka tu na kuweka sheria ambazo zinawakandamiza natives na kuwanufaisha wageni, na hili ni tatizo la watanzania kuwapapatikia sana wageni kuliko watanzania wenzao.

Wakati mwingine mnapojaribu kutoa maoni yenu muwe na adabu, sio mnaropoka tu kama zimewafyatuka. Afterall hapa ni mjadala wa wanamara kwa ajili ya kutafuta namna ya kujikwamua na madhila tuliyonayo, sasa nyie mliopata nafasi ya kujikwamua kupitia rasilimali zetu mnatakiwa muonyeshe heshima na si madharau kwani kwa kufanya hivyo hatutahitaji tena ushauri wako katika hili, nenda tu ukajenge/ukaendeleze huko kwenu utuache na Mugumu yetu, sisi wenyewe tutaweza kuifikisha mahali tunapotaka.
 
safi sana mkuu, inapendeza kuongea kwa vitendo, tunasubiri mwaliko wako ili tuweze kuchangia japo mawazo ni kweli kile ki-mkoa kimekaa vibaya kidogo na ni jukumu letu kuweka mambo sawa, wana siasa wamekuwepo siku zote na kamwe hawana nia ya kufanya chochote pale zaidi ya kuomba kura kila baada ya muda
 
Mara itajengwa na wana-Mara wenyewe,achana na wadandiaji.Namba zangu za simu ni 0782 577 006,tutafutane ndugu tuzungumzie harakati zetu.
 
Saganka angusha hiyo draft ya katiba watu watoe comment rather than rushing na kusajili umoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…