Ngoja nikukimbize chap chap.
Honda Fit kwa Japan, ni Honda Jazz kwa mataifa mengine ni gari flani wanaliita subcompact hatchback kutoka Honda. Hadi leo 2024 kuna generations nne za hii gari, kutokea ya kwanza 2021.
Hii gari toka ianze tengenezwa 2001 imetokea kupendwa sana. Na ni moja ya gari ambayo imewahi kumshinda Corolla kwenye mauzo ya mwaka, tena sio mara moja. Ata ukiingia mfano Beforward, ili ndio top selling car la Honda.
Hii gari inapendwa sana kwanini, kwasababu ni economy, cheap, kagumu, kana nafasi (kuna msemo unasema anything can fit on Honda Fit), na kanamuonekano mzuri.
Ukiingia mitandao ya kuagiza magari JP, utakuta zipo Fit za aina nne (4). Honda Fit, Honda Fit Hybrid, Honda Fit Shuttle na Honda Fit Shuttle Hybrid. Tutajaribu ziongelea kidogo kama kuna muda.
1st Generation 2001 hadi 2006: Code GD & GE
Tuseme ilikua simple, ina engine ya 1.2L, 1.3L na 1.5L CVT transmission.
Hili gari ukikunja seat za nyuma ukazilaza, unaweza weka kabati kule nyuma, kswasababu zile seat zinalala.kweli kweli na ukichukulia wameweka tank la mafuta seat za mbele ili nyuma kuwepo na nafasi kubwa ukitaka beba mzigo.
Kuzipata 1st generation online ni changamoto kidogo, ila nyingi CIF ni kuanzia $3000.
Ushuru wa TRA ni kati ya 5.5 mil hadi 7 kwa hapa nimechukua ya 2002 nimepata 5.9 mil.
Kua makini kwenye Model hapo izo herufi GD ndio first gen iyo.
Ukipiga simple math, unakuta jumla mil 12 - 13 hivi.
Ushauri wangu: Sio nzuri kwasababu ya zamani sana hafu bei kali, bora uende 2nd gen. Naomba niiongelee kwenye comment ya chini yake hapa.