Kwa watumiaji wa Tecno tu

Kwa watumiaji wa Tecno tu

Fazz

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2019
Posts
578
Reaction score
1,241
Ndugu zangu, sisi watumiaji wa Tecno tumekuwa tukionekana cheap sana kutokana na simu zetu za Tecno kudharaulika kana kwamba ni za kimasikini tofauti na wale wanaotumia iPhone, Samsung ama sijui Huawei, Oppo na nyinginezo nyingi.

Leo nataka niwaambie faida za kutumia Tecno:

1. Tecno inauzwa kwa bei nzuri ambayo yoyote anaweza kuimudu tofauti na nyingine.

2 .Tecno inafanya yote ambazo simu nyingine zina uwezo wa kuyafanya.

3. Tecno inatengenezeka kirahisi na bei poa kuliko misimu mingine, pia spea zake zipo tele.

4. Tecno imepewa uwezo wa kustahimili mikiki mikiki. Tecno yangu, Camon X ishaanguka zaidi ya mara hamsini na bado naitumia nzima.

5. Tecno inapopotea au kuibiwa presha haiwi kubwa kama zilivyo simu nyingine kama iPhone na Samsung za bei mbaya.

Hizo ni baadhi ya faida za Tecno na zipo nyingi sana, tunaelewana? Tupo juu kama upepo wa kisulisuli.
 
TECNO yangu ina miaka 3 na miezi 6 tangu niinunue dukani bado inapiga kazi hadi Twitter wamenionea wivu wakaniban kutumia App yao.
Kawatembezee kipigo makao makuu
 
[emoji3][emoji3]
TECNO yangu ina miaka 3 na miezi 6 tangu niinunue dukani bado inapiga kazi hadi Twitter wamenionea wivu wakaniban kutumia App yao.
 
[emoji3][emoji3]
Ndio hivyo mkuu, tunalazimishana kununua simu kwa mtindo wa kubadili specifications za App aisee.

Yaani App wanazitengeneza kwa aina fulani za simu ambazo zinakuwa ni matolea ya hivi karibuni
 
Tecno ni Uchafu kama uchafu mwingine, Cm yoyote ya MTK ni uchafu
 
Back
Top Bottom