Kwa watumiaji wa tigo

TIMING

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2008
Posts
28,186
Reaction score
15,549
Inaonekana leo [tar 19/8/2009] tIGO imechoka na mitambo yake imegoma kutoa sauti... watu hawasikilizani na sometimes simu haziiti kabisa. ni tatizo la zaidi ya masaa sita na wale watumiaji wa mtandao huu ni mateso matupu wakati sekunde za watu zinaliwa... pole

CHEAP IS EXPENSIVE
 
Last edited:


suala la mtandao kusumbua linatokana na u cheap wake? mbona kuna wakat zain ilikuwa inasumbua sana, hata voda pia huwa inasumbua.
 
Wapinzani wa tiGo utwajua tu....Fidel80 uko wapi?
 
hahaha simu ya watu, leo wako hivyo kesho ni voda na zain. nafikiri huyu ana mpango wa kutudhalilisha tu.
 

Suala la mitanddao kusumbua mara moja moja huwa linatokea, hasa iwapo jamaa wanafanya ukarabati ama wa tarakilishi ama wa mitambo yao ya kurushia mawimbi. Hii ni kwa mitandao yote. Ni suala la muda tu! Cha kufanya ni kuwajulisha watu wa huduma kwa wateja, iwapo kuna shida.
 
of course hizi ni machine unategemea zifanye kazi 24/7 bila kusumbua? mwili wako wenyewe unasumbua sembuse mitambo iliotengenezwa na binadamu?haya wapinzani wanochunwa na kujidai jeuri hamuna lolote, endeleeni kuchunwa na umaskini hautawaisha
 
yaani aliye-post hiyo kitu kuhusu tigo inaonekana ana chuki binafsi na mtandao huo...he thinks just becoz he's on voda/zain then automatically he belongs to a certain class in the society...yaani huu ndo umaskini wa fikra.network cheap hapa mjini ni zantel kwanza ikifuatiwa na tigo...na mtu yeyote mjanja lazima atakuwa kwenye hiyo mitandao ya ukweli...
 
Bila shaka mkuu, itakuwa ni kacellular kake tu......mi nalonga kama kawa..

Hivi vi-handset vya kichina navyo vina mambo...!
 
Duh, yaani wajameni mlivyonishambulia.... kama naoga nje!!!???

Nisingejua kwamba tIGO ina matatizo kama nisingekuwa na line, hilo la simu ya kichina labda maana natumia NOKIA N70 kwahiyo labda ndio yenye matatizo... Labda tujiulize pia, ni mimi peke yangu tu alipata tatizo hilo leo??? au tunaingiza biashara hata kwenye reality??

Lengo ni kutoa changamoto tIGO wa-improve, sasa kama mnaridhika na shortfalls sawa, mie sikuridhika... Yakinikuta za Voda au Zantel pia ntasema jamani

AU NYIE TIGO ZENU ZIKO POA??
 

Wateja wanastahili huduma bora. Si haki kuwakata watumiaji pesa wakati service hawaipati. TCRA bado ina kazi kubwa ya kufanya hasa elimu juu ya haki kwa wateja wa simu.

Wachangiaji wengi naona wanasema ati ni kawaida, itakwisha na hata operators wengine huwa na matatizo hayo. Lazima tufike mahali tuseme no kwa poor services (especially when they charge us for such poor services).Kama kuna matengenezo(planned) wanatakiwa kutoa taarifa au kufanya matengenezo kipindi chenye low traffic (say usiku).
 
tigo zetu????...Wewe endelea kutumia mitandao ya mafisadi uendelee kuwa changia...

Crashwire, jaribu kuchukua bandiko lote na si vipande ili ulete ligi ya kombe la senene; nimeeleza wazi kwamba natumia mtandao wa tIGO na nikauliza kama zenu poa... au hili nalo kosa??

the best way to help someone is understand the person
 

Thanks kwa kunielewa, if we dont fight for our rights and benefits, tutaendelea kuonekana wapinzani tu!!

The aim is to keep providers on their toes so that they offer us the best services

Pamoja
 
Mimi mbona sijapata tatizo? ebu fuatilia labda ni simu yako tu.
 
Mimi mbona sijapata tatizo? ebu fuatilia labda ni simu yako tu.

mimi ni mmoja ya mteja wa Tigo niliyepata tatizo siku ya leo. Mara ya kwanza nilifikiri ni simu yangu ina matatizo. Lakini tatizo liliendelea hata baada ya kubadilisha simu.

Tatizo hapa ni taarifa kwa wateja, kama mtoa huduma ni wajibu wake kutoa taarifa pale anapokuwa na matatizo na mtandao wake. Mbona kuwa rahisi kutuma matangazo ya biashara (promotions) kwa SMS, kwanini isiwezekane kwa hili. Na hii nazungumzia kwa mitandao yote ya simu Tanzania si Tigo peke yake. Leo ni Tigo, lakini hata ikitokea kwa Vodacom au Zain hawana utamaduni wa kuwapa wateja wao taarifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…