Kwa watumiaji wa tigo

frakitosho

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2012
Posts
802
Reaction score
256
Wana jamvi baada ya kuongea na simu tigo kwa tigo nimepata ujumbe ufuatao "Umetumia sekunde 143, umelipia sh 236.67. Salio lako ni 450.93. LONGA BEI MOJA MITANDAO YOTE TZ KUANZIA THUMNI". Kilichonishangaza hapa ni kwamba kimahesabu hii gharama ni sawa na shilingi 1 na senti 65 kwa sekunde lakini wao wanatudanganya eti longa kwa bei moja mitandao yote kuanzia thumni. Tigo acheni uhuni wa waziwazi. Hata ukijumuisha makato ya kodi haiwezekani thumni ambayo ni sent 50 ipande hadi sh. moja na senti 65. Wana jf tukemeeni kwa nguvu utapeli huu. Acheni utapeli ninyi Tigo.:nono:
 
he he he he he he he he he sasa si ni sh 1 bila vat mkuu...hebu piga 18% vat utapata mpango mzima....
 
Tigo sasa hivi natumia kwa tigo pesa tu. Mambo ya kulonga mitandao yote nimehamia Airtel ambayo yanitosha....

Tigo wako mashakani na ofa ya Airtel.....Yatosha!!
 
Tigo sasa hivi natumia kwa tigo pesa tu. Mambo ya kulonga mitandao yote nimehamia Airtel ambayo yanitosha....

Tigo wako mashakani na ofa ya Airtel.....Yatosha!!

Ni kweli kabisa mkuu hata mimi ngoja nikanunue line ya airtel yatosha niachane na tigo
 
he he he he he he he he he sasa si ni sh 1 bila vat mkuu...hebu piga 18% vat utapata mpango mzima....

Hata kama ikiwa sh 1 kwa sekunde then ukaweka 18% ya VAT ilitakiwa iwe shilingi moja na sent 18 na sio sh moja na sent 65 kama walivyonikata. Ni wezi wa mchana wanaiba bila aibu wanadhani kila mtanzania hajui hesabu. shit.
 
mkuu mi sio mtaalamu wa mambo ya kodi lakini jaribu kuuliza wataalamu aisee.....
 
Heading ilinichanganya kidogo maana mimi ni mtumiaji mzuri wa TIGO, lakini sio mnayozungumzia.
 
Kaka mbona Tigo rahisi hivyo we unalalamika?
Yaani kuonjeshwa sekunde moja kwa Tshs hazizidi hata 2/= unaona ghali??

Wengine wanalipia mpaka kwa kuhonga Magari just for that tiGO.
 
switch to airtel mkuu mi natosheeeeka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…