frakitosho
JF-Expert Member
- Dec 13, 2012
- 802
- 256
Wana jamvi baada ya kuongea na simu tigo kwa tigo nimepata ujumbe ufuatao "Umetumia sekunde 143, umelipia sh 236.67. Salio lako ni 450.93. LONGA BEI MOJA MITANDAO YOTE TZ KUANZIA THUMNI". Kilichonishangaza hapa ni kwamba kimahesabu hii gharama ni sawa na shilingi 1 na senti 65 kwa sekunde lakini wao wanatudanganya eti longa kwa bei moja mitandao yote kuanzia thumni. Tigo acheni uhuni wa waziwazi. Hata ukijumuisha makato ya kodi haiwezekani thumni ambayo ni sent 50 ipande hadi sh. moja na senti 65. Wana jf tukemeeni kwa nguvu utapeli huu. Acheni utapeli ninyi Tigo.:nono: