Kwa wazazi ambao wanapenda kukuza vipaji vya watoto wao

Kwa wazazi ambao wanapenda kukuza vipaji vya watoto wao

Qifrishy

Senior Member
Joined
Jul 6, 2014
Posts
169
Reaction score
42
AFRISOCCER TANZANIA
TANGAZO
AFRISOCCER WEEKLY SOCCER CLINICS COMING

SOON!

"Mwandikishe mtoto wako kwa ajili ya mafunzo
ya soka kwenye Soccer Clinics za kila wiki -
Jumamosi na Jumapili".

Umri ni kati ya miaka 8 hadi 14! Kuanzia
Novemba 2014.

Watoto watafundishwa kucheza mpira,
kuendelezwa na kusaidiwa kufikia malengo yenye
kukuza vipaji vyao kutoka kwa waalimu wenye
ujuzi na mafunzo ya kukuza vijana ambao
walicheza na kusomea ukocha wa vijana nchini na
nje ya nchi.

Mafunzo yote yatakuwa yakirekodiwa
na kuhifadhiwa katika Youtube akaunti ya
Afrisoccer na kuwa mlango wa fursa nyingine kwa
vijana washiriki.

Faida ambazo mtoto atazipata kwa kushiriki
kliniki ni pamoja na:

• Nafasi ya kuonana na wachezaji wa zamani na
sasa ambao wamecheza kwa mafanikio kwenye
vilabu tofauti tofauti na Taifa Stars ambapo
watapata mafunzo, mbinu na hamasa ya
kujiendeleza kisoka kutoka kwao

• Nafasi ya kutengenezewa video kwa mchezaji
mmoja mmoja ambao wataonyesha jitihada na
kipaji na kupendekezwa na kocha

• Nafasi ya kuingia mkataba na Afrisoccer
Consulting Ltd ya kusimamiwa maendeleo na haki
za mchezaji baada ya makubaliano na mzazi wa
mchezaji

• Nafasi ya kuunda timu ya Afrisoccer ambayo
kwa siku za usoni itashiriki mashindano
mbalimbali ya vijana nje na ndani ya nchi
hususani Gothia Cup

• Nafasi ya kumulikwa na maskauti wa soka
duniani kwote na washirika wengine wa Afrisoccer
Marekani na Ulaya hususani nchi za Scandinavia
kwa ajili ya majaribio na fursa nyingine za
kimichezo kwa washiriki wenye vipaji na jitihada.

• Nafasi ya kushirki michezo mingine ya watoto
na kuunda marafiki.

Wazazi tukumbuke kuwa Soka ni kazi, ni ajira na
fursa kwa watoto wetu. Ungana na Afrisoccer
kusaidia kulea vipaji vya watoto wetu.

Taarifa
zaidi juu ya mahali, ratiba na utaratibu wa
kushiriki zitafuata baada ya kupata idadi kamili ya
waliojisajili!

Tuandikie:

E-mail: [email protected]

Au

Tupigie:

Simu: +255 655 22 00 39 Au +255 654 68 74 03.
 
Back
Top Bottom