Wazazi wengi siku hizi hatuna muda na watoto wetu... Watoto wamekuwa ni wa wadada wa kazi na walimu, makuzi ya mtoto kiakili na kimaadili yanahitaji uwepo na ukaribu wa mtoto kuliko mtu mwingine yeyote yule.
Pamoja na harakati za kimaisha lakini ni vema ni muhimu na kuna wakati kutenga muda wa kukaa na familia yako ili kile ukitafutacho kiwe na manufaa na baraka mbeleni.
Dada wa kazi ana sehemu yake na majukumu yake ambayo ni 1/4
Mwalimu ana sehemu yake na majukumu yake ambayo ni 1/4 pia
Mzazi ana majukumu yake ambayo ni 1/2
Kwahiyo kama mzazi usibweteke nusu nzima ya malezi ya mtoto inakuhusu wewe.
Hili jambo nimekuwa najaribu kusema lakini wazazi wetu yani wakwe na mama zetu huchangia sana kuumiza watoto ktk eneo hili kwa kisingizio mtoto anahitaji joto mtoto huwa hasikii joto wanashindwa kuelewa dar ni tofauti pengine na mkoani ulipozaliwa wewe au bibi huyo alipokuzia watoto wake wengine unaenda clinic daktari anakushangaa jinsi ulivyomjaza mtoto nguo nyingi kabaki macho tu.wazazi tuwe makini hawa ni wakubwa zetu ila panapobidi kuwaelewesha tufanye hivyo vinginevyo ni sisi ndio tunakuja kupata shida na watoto wetu badae.
Hili la chakula aina moja teh ni shida utadhani kuna ratiba ya kupewa uji, watoto tunawaonea kuwapa uji kila siku kila siku ndo maana hata wanakua wanasumbua kuunywa
Chai ya tangawizi mtoto mdogo atakubali kunywa kweli?Mshana ungefafanua vizuri kuhusu Asali, nijuavyo ni hatari sana kumpa mtoto mdogo Asali mbichi. At least akishazidi miaka mi5.
Kuhusu Pneumonia inasababishwa zaidi na baridi. Ukimwona mtoto anatetemeka sanaaa wakati wa baridi usitumie dawa yoyote zaidi ya chai ya rangi yenye tangawizi kidogo then mfunike alale. Akiamka yupo shwariii.
Shukran mshana jr kwa ubunifu wa mada hii.
Umri gani mzuri?Maalum kwa watoto wa kiume
Si vema kumuwahisha tohara mtoto. ..hii ni kwa faida yake ukubwani, tohara inayowahi husababisha vibamia
Kwa wale wenye watoto wanaosoma
-ni lazima na ni muhimu kumpa namba zenu wazazi au kuziandika kwenye begi lake ni muhimu na zimesaidia wengi
-kumuonya tabia ya kuombaomba na kuwa makini na watu asiowajua. ..watoto wengi wanaopotea hupotea kwa staili hizi
Hawa watoto wanaosoma ni vema kuzifuatilia nyendo zao kwa karibu tabia zao marafiki walionao na vitu walivyo navyo kwenye mikoba na vyumbani mwao
Teh sijui kwanini uji ndio ratiba zetu wamama sijui nani alifundisha hii, huwa unawapa nini badala ya uji?Hivi uji ni lazima kwa watoto? Mi sijawahi kuwapa watoto wangu kabisa.
kumbeeee..Maalum kwa watoto wa kiume
Si vema kumuwahisha tohara mtoto. ..hii ni kwa faida yake ukubwani, tohara inayowahi husababisha vibamia
Nadhani ni kama ulivyosema hapo juu, NI CHAKULA RAHISI kwa gharama na maandalizi pia. Ukiacha wale ambao hujitahidi na unga wa lishe+butter+maziwa, ukiwa na unga wa mahindi tu na chumvi tayari mtoto anaacha kulia njaa.Teh sijui kwanini uji ndio ratiba zetu wamama sijui nani alifundisha hii, huwa unawapa nini badala ya uji?
kumbeeee..Maalum kwa watoto wa kiume
Si vema kumuwahisha tohara mtoto. ..hii ni kwa faida yake ukubwani, tohara inayowahi husababisha vibamia
Ooh kumbe hata asubuhi anaweza kuanza na msosi heavy mi huwa nadhani vema kuanza na vitu laini kama vile maziwa na yai, au supu au uji kumbe hata ndizi samaki anakula tu, ahsante kwa experience mupyaNadhani ni kama ulivyosema hapo juu, NI CHAKULA RAHISI kwa gharama na maandalizi pia. Ukiacha wale ambao hujitahidi na unga wa lishe+butter+maziwa, ukiwa na unga wa mahindi tu na chumvi tayari mtoto anaacha kulia njaa.
Mi huwa nawapikia chakula kabisa kama wali, viazi, ndizi, ugali na mboga kama nnazokula mie (samaki, nyama, za majani n.k). Wa kwanza nilimsagia sana mchanganyiko wa chakula ila last born kala bila kusagiwa, sema tu mwanzo nilikuwa navifanya vilaini. Alafu ilikuwa rahisi maana last-born alianza kula kwa kuonja tu kidogo kidogo maana bado alikuwa ananyonya muda wote mpaka alivyofikisha miezi 10 ndo akaanza kula kwa kushiba chakula.
Umri sahihi ni miaka mingapi?Maalum kwa watoto wa kiume
Si vema kumuwahisha tohara mtoto. ..hii ni kwa faida yake ukubwani, tohara inayowahi husababisha vibamia