Kwa wazazi na walezi: Mada maalum ya watoto

Kwa wazazi na walezi: Mada maalum ya watoto

Tatizo langu ni kwamba mtoto wangu kazaliwa tarehe 8 mpaka leo tarehe 11 upatikanaji wa maziwa kwa mke wangu ni mdogo sana ,JE NINI SULUHISHO LA MAMA WATOTO ILI ATOE MAZIWA HARAKA? mshana jr
Kuna vidonge vyake lakini nashauri onana na daktari kwa ushauri na maelekezo
 
Mkuu vinaitwaje nikamnunulie?
1471021001343.jpg

Mkuu vinaitwaje nikamnunulie?
 
Hapo kwenye lishe ya mtoto wa siku moja mpaka miezi sita, maziwa ya mama peke yake hayatoshi. kuna haja ya kuongezea uji mwepesi kadiri mtoto anavyokuwa, maana watoto wengine jinsi anavyokuwa maziwa ya mama hayamtoshelezi. utakuta mtoto hapati usingizi vizuri sababu ya kutokushiba vizuri
Acha uwongo wa kupotosha watu wewe nahisi utakuwa mtaalamu wa lishe usiye jielewa kadanganye wa zazi wa kijijini kwenu.
 
Acha uwongo wa kupotosha watu wewe nahisi utakuwa mtaalamu wa lishe usiye jielewa kadanganye wa zazi wa kijijini kwenu.
solog huku sio jukwaa la siasa kwahiyo reply za namna hii hazina nafasi kwenye hii mada, tunachofanya hapa tunabadilishana uzoefu na kupeana maarifa, na hata kama ni kupingana ama kukosoana si kwa jinsi hii ya kwako
Ukiwa mstaarabu na muungwana unaweza kuomba radhi
 
Maalum kwa watoto wa kiume
Si vema kumuwahisha tohara mtoto. ..hii ni kwa faida yake ukubwani, tohara inayowahi husababisha vibamia
Havina uhusiano kuna watu wazima na magovi yao bado wana vibamia ukubwa wa uume unatokana na lishe bora na wengine urithi kutoka kwa wazazi wao.
 
Mshana Jr hii inategemea na maumbile tu ya mtoto tangu anazaliwa was kwangu nilimfanyia akiwa na 2weeks,sasa hivi ana 4yrs na mashine yake ni ya uhakika hadi namuonea huruma huyo mkwe atakayeimiliki.
wewe mkatili 2 week nouma sana
 
mdogo wangu kacheza michezo ya hatar sana na waume wa watu sasa kajifungua kwa operation sasa nahisi alikuwa anatoa 0658/0715
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
nashukuru nmesoma maelezo yote nimeelewa nimeamua kufuatilia thread zote kwa sababu mwanangu alizaliwa 17/07/2016 sasa anakarbia mwezi alipata mafua na kikohozi sasa tukanunua codrin lakin haijamsaidia ila kuna doctor alikuwa kashaur kununua amplicox syrup kama spelling sijakosea ila bado haijanunuliwa sasa
 
Nadhani inawezekana kabisa kwakuwa kuna baadhi ya upasuaji hufanyika chini ya umri huo

Hapo kwenye lishe ya mtoto wa siku moja mpaka miezi sita, maziwa ya mama peke yake hayatoshi. kuna haja ya kuongezea uji mwepesi kadiri mtoto anavyokuwa, maana watoto wengine jinsi anavyokuwa maziwa ya mama hayamtoshelezi. utakuta mtoto hapati usingizi vizuri sababu ya kutokushiba vizuri
 
Mtoto Wangu ana miezI 7, amepata malenge lenge sehemu ya mapajani yaani yakipasuka yanaota mengine hili linaweza Kuwa tatizo gani? Na dawa gani nimpatie
 
Mtoto Wangu ana miezI 7, amepata malenge lenge sehemu ya mapajani yaani yakipasuka yanaota mengine hili linaweza Kuwa tatizo gani? Na dawa gani nimpatie
Inaweza kuwa ni mzio wa chakula ama kinywaji the best wasiliana na Dr bingwa kuepuka guess works
 
Back
Top Bottom