kwa watoto wanaosumbua kula kuna dawa inaitwa pharmactin
hii dawa huwa inasaidia sana kumuongezea mtoto hamu ya kula ila kwa experiency nilo nayo ukiandikiwa dozi ukaanza kumpa akianza kuchanganya kula usiendelee na dozi maana atakuwa msumbufu wa kuhitaji kula
Ushauri wa pili kama unasimu na unamuachia mtoto kuangalia video iweke kwenye flight mode
muwekee mtoto wako education videos za shule za chekechea kuliko kumuwekea nyimbo za bongofleva au video za ajabu ajabu. hili ninaushuda nalo kwa mwanangu niliye naye kwa sasa ana miaka miwili lkn anajua namba hadi 20 na anafahamu ABC...Z kutamka akiziona na kuziandika
mkaririshe mwanao namba moja wapo ya mzazi hii itakusaidia sana
mlishe mwanao samaki kwa wingi hasa sato au sangara inasaidia ukuaji wa ubongo na akili kwa mtoto
tenga muda wa kucheza na watoto wako hii inasaidia kumjengea mtoto mapenzi ya wazazi na kujiamini na kutokuwa na nidhamu ya woga
mjengee mwanao mazoea ya kuhoji na kuweza kutoa sababu ya anachohoji
hata kama uwe busy vipi jitahidi kuwatoa wanao out mkiwa wazazi wote wawili baba na mama. Jitahidi walau kula pamoja na watoto wako hata chakula cha jioni.
usigombane na mkeo au mumeo huku watoto wanashuhudia.
usimuongelee mabaya mkeo au mumeo mbele ya watoto.
Jitahidini kila mara watoto wawaone wazazi mna furaha.
Salini pamoja na watoto wenu kwa wakristo waweza teua mtoto aongoze sala
kwa waislamu kama wasalia nyumbani baba ongoza sala ila ukimaliza mwambie mtoto aombe dua.
mpongeze mpe zawadi mtoto pindi afanyapo jambo lolote zuri.
Afya ya mwanao ni muhimu fuatilia afya ya mwanao na tabia za mwanao mueleze wajibu wake ni nini kama mtoto na wewe kama mzazi wajibu wako nini
Mueleze mali ulizonazo ni zenu ninyi wazazi anatakiwa yeye baadae atafute mali zake atapokuwa mkubwa.
unapofikiria kuchepuka au kumfanyia vitimbi mwenzio kwenye ndoa ujue mwisho wa siku mtaachana na hakika nakiri Hakuna Mama kama mama na hakuna baba kama baba. hivyo mwanao hatopata malezi bora kama kutoka kwa baba halisi au kwa mama halisi, kwakuwa hakuna mzazi halisi apendae mwanae kuwa na mwisho mbaya.
Usimueleze mwanao matatizo ya baba yake au mamaake akiwa bado mdogo badala yake tatue matatizo na tofauti zenu kabla hamjapanda kitandani kulala. maana penye maudhi shetani hutawala mwaweza fanya tendo la ndoa mkazaa shetani badala ya binadamu
Mshana Jr anaweza tolea ufafanuzi hili.
Ikumbukwe mtoto ni wako anapokuwa mdogo lkn akikua huwa ni wa jamii inayomzunguko lea mwanao kwa maadili mazuri ili tuwe na jamii Bora
Kumbuka hakuna mtu yeyote atayekulelea mwanao kama wewe mwenyewe mzazi.
Kumbukeni kuna maisha baada ya watoto wasisitize wanao kuheshimu kila binadamu duniani
Kama hakuna ulizima usimpeleke mwanao boarding school akiwa vidudu na shule ya msingi, hii inaweza sababisha mtoto akakosa mapenzi na mzazi.
msikilize mwanao usipende kumkatisha anapokuambia jambo hata kama nila kitoto au kipuuzi msikilize then shauri au onya au pongeza kutegemeana na jambo lenyewe. usipofanya hivyo utasababisha asijekukuambia lolote na akajenga nidhamu ya woga kwako.
Mwambie mwanao akuheshimu ila asikuogope