kadendu
JF-Expert Member
- Mar 30, 2014
- 645
- 496
Waziri mkuu kwa niaba ya wanakijiji wa Mtera staff mpwapwa DODOMA nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kukupa afya njema na kuendelea na majukumu yako ya kitaifa.
Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa unyenyekevu mkubwa naomba nifikishe malalamiko yetu kwako juu ya mradi wa maji ambao umehujumiwa kwa muda mrefu Sana na baadhi ya viongozi huko wilayani mpwapwa lakini pia nimpongeze mh mkuu wa mkoa aliyehama ndugu Antony Mtaka kwa kuwa bega kwa bega na sisi kufuatilia mradi huu, katikati ya mwaka huu alikuja hapa Mtera na kuwataka viongozi wa wilaya ya Mpwapwa wahakikishe mpaka tarehe 25 Sept 2022 wawe wamemaliza mradi na atakuja kukagua kwa bahati mbaya kabla ya hiyo tarehe akawa amehamishwa mkoa na kwenda Njombe hivyo imepelekea mradi umezorota kama mwanzo.
Kitu kinachotushangaza mh Waziri wa maji siku za karibuni alifanya ziara ya miladi ya maji wilayani Mpwapwa kwa maksudi viongozi wa wilay yaMpwapwa walimkwepesha kwa maksudi asije kijijini kwetu kwani tungehoji habari ya mradi wa maji badala yake akaishia Kijiji Cha jirani cha Chipogolo.
Tunajua ilikuwa ni hujuma au mbinu chafu ya maksudi Sasa mh waziri mkuu tunakuomba uchunguze ni kwanini muhandisi wa wilaya ya Mpwapwa mradi wa billion na pointi 7 vifaa vya mradi ananunua yeye mwenyewe kama anafanya shopping mnadani wakati tunafahamu taratibu ya manunuzi vifaa vya Serikali na kwanini atutishie wananchi atakae hoji atamfunga.
Sisi hatuogopi kufungwa kwa kuhoji pesa za Serikali kwani ni yetu Ila tunaomba kabla hajatufunga uje Mtera tukueleze bayana namna mradi unavyohujumiwa mchana kweupe na tunahisi mtandao ni mpana na Kuna mkubwa mmoja Ila tunajua wewe utammudu tu sekunde karibu waziri mkuu wetu Mtera Ili mbivu na mbichi zijulikane takutakia majukumu mema ya ujenzi wa taifa.
Ni Mimi Kadendu katika ujenzi wa taifa.