Kwa waziri (serikali), na raia - uhaba wa mafuta ya kupikia

Kwa waziri (serikali), na raia - uhaba wa mafuta ya kupikia

Thinker96

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2011
Posts
349
Reaction score
139
Wasalaam watu wa Mungu,
Pasi na kuchelea twende sanjali kwenye mada.

Uhaba wa mafuta ya kupikia kero ya miaka mtawalia. Ni fursa ya uwekezaji kwa biashara ya muda mrefu hata kwa mtaji mdogo au mkubwa.
Mchanganuo.

Mahitaji ya mafuta Tanzania kwa sasa ni 600,000MT na uzalishaji ni ~200,000MT kwa hiyo kuna uhaba wa metriki tani 400,000.

Mazao yanayotoa mafuta hapa Tanzania ni Alizeti, Michikichi, Karanga, Soya na mengineyo.

Nitajikita kuelezea mchikichi kwa kuwa hudumu mpaka miaka 35+ toka limepandwa na ndo hutumika kutengeneza mafuta mfano Korie.

Ili tupate kiasi cha 400,000MT inabidi tupate miche ya Michikichi 12Milioni ambazo zinaweza kupandwa kwenye eneo la 800km² na ukubwa wa nchi yetu ni ~948,000km²

Mkulima binafsi ukilima heka moja nitaelezea mbegu ya Tenera katika maelezo yangu ambayo huanza kuzaa baada ya miaka mitatu mpaka thelethini na zaidi ni kuzaa tu kwenye msimu.

Heka moja unaweza ukapata zaidi ya Tani moja (Lita 1,100).
Uwekezaji full wa serikali kwa hizo 800km² ni $280Mil ila partially kwa kutoa mbegu na elimu haizidi $80Mil. Hii itaondoa kabisa adha ya mafuta ya kupikia na kushusha bei na kumnufaisha mwananchi na kutengeneza ajira 160,000.

Kwa mtu binafsi haizidi Mil2-7 kwa heka itategemea na unalimia wapi. Mbegu za Tenera hybrid zinapatikana TARI hasa ya Kigoma ndo wa kuulizwa.

Kwa nchi inaweza kuagiza Indonesia au Malaysia kwani kwa uwezo wa TARI tutachelewa ni kiwango kikubwa.

Uhaba wa mafuta tukiendelea hivi kwa kuzalisha theluthi ya mahitaji kama nchi itapata hasara kwa BoT, BoP na pia kwa baadae italeta madhara kwa mfumuko wa bei wa kuzidi kwa kuwa kufika mwaka 2100 tunategea kuwa na population ya watu zaidi ya Mil200.

Maeneo ambayo Mchikichi unakubali Kigoma, Mbeya, Songea, Tanga, Pwani, Dar Es Salaam, Lindi, Mtwara, Katavi, Rukwa
Maelezo ni mengi ila nimeyaminya sana ili nisiwachoshe wasomaji wenzangu. Nipo tayari kurekebishwa inapobidi na kuulizwa swali.

Ahsante
 
Chambuzi maridhawa kabisa... Changamoto ya uhaba wa mafuta inaenda sambamba na uhaba wa byproducts zake kama Mashudu ambayo hutumika kulisha mifugo.
 
Na huu ndio ukweli wenyewe kabisa.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom