Tetesi: Kwa waziri wa Afya-je Ni kweli wizara yako ina uhaba wa chanjo kwa watoto wachanga?

Tetesi: Kwa waziri wa Afya-je Ni kweli wizara yako ina uhaba wa chanjo kwa watoto wachanga?

Bursting

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2020
Posts
289
Reaction score
520
Kwako waziri wa Afya Ummy Mwalimu, pole na majukumu ya kazi. Kuna tetesi nimezipata kutoka kwa nesi mmoja ambaye hakupenda kutaja kituo chake cha kazi akielezea namna hali ambavyo imekuwa mbaya katika vituo vya afya nchini baada ya kuwepo kwa upungufu wa chanjo kwa mtoto mdogo azaliwapo ambapo huwa anachanjwa mara azaliwapo! Ameendelea kueleza kuwa kutokana na kukosekana kwa sindano hiyo ambayo naamini unajua umuhimu wake kwa mtoto azaliwapo nasikia imefikia hatua mpaka watoto wamefikisha mpaka miezi 2 bila kupata hiyo chanjo, swali langu kwako ni je haitakuwa na madhara yoyote kwa mtoto akikosa hiyo chanjo??

nawasilisha kwa waziri husika
 
Back
Top Bottom