Kwa Waziri wa Fedha Dr Mpango: Maoni kuhusu vikwazo katika kufanya biashara Tanzania

Mfiaukweli

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2018
Posts
5,636
Reaction score
8,777
UTANGULIZI
Wakuu; hivi karibuni Waziri wa Fedha Dr Mpango alialika watu kutoa maoni yao kuhusu mambo wanayoyaona kuwa ni kikwazo (au vikwazo) kwao katika kufanya biashara na akaahidi kuwa serikali itayafanyia kazi maoni hayo. Ni kwa sababu ya wito huo (najua watu wa serikali hupitia hapa) natoa maoni yangu na kuomba wadau wengine nao watoe maoni yao.

Angalizo: Naomba tutoe maoni kuhusu vikwazo vilivyopo kwenye kufanya biashara (kama kuna mtu anaeona kila kitu kinaenda sawa HANA SABABU ya kutoa hizo "sifa" zake kwenye uzi huu tafadhali). For once let's be serious.

MAONI
Baada ya utangulizi huo, naomba nitoe maoni yangu kama ifuatavyo:

1. Jambo kubwa kuliko yote ambalo limekuwa KIKWAZO kikubwa katika kufanya biashara (hasa tangu serikali hii iingie madarakani) ni kufanya maamuzi bila kuzingatia sheria. Mhe.Waziri, HAKUNA kitu wawekezaji wanakiangalia (kabla ya kuwekeza) kama certainty (uhakika) kwenye kanuni zilizopo nchini. Mnapotoa matamko yanayofuta sheria na taratibu zilizokuwepo instantly zinamfanya mfanyabiashara asijue atarajie nini kesho (maana alichopanga kukifanya leo kinaweza kukatazwa kesho na hatafidiwa hasara atakayoipata).

Kitu cha pili kinachohusiana na utawala wa sheria ni hii tabia/dhana iliyojengeka sasa hivi kuwa serikali inaweza kumuonea mtu lakini yenyewe ikawa na kinga ya kushtakiwa (na hata ikishtakiwa na ikashindwa hailazimiki kuwajibika kumfidia muathirika). LAZIMA turudishe na kuimarisha investors' confidence kwa nchi hii (ambayo kwa sasa hivi naamimi hata wewe mwenyewe Mh. Waziri unajua kuwa haipo).

2. TRA wafanye kazi zao kwa haki. Sasa hivi imezuka tabia ya kubambikia madai ya kodi (huku maafisa wa TRA wakijua fika kuwa HAKUNA hata chembe ya ukweli kwenye hayo madai) ili tu mfanyabiashara alazimishwe kulipa jspo theluthi ya madai hayo bandia (maana sheria inamtaka mlipa kodi kulipa theluthi moja ya kile alichodaiwa - hata pale kunapokuwa na ushahidi dhahiri kuwa madai si sahihi ili objection yake isikilizwe). Sheria hii inakuwa abused sana hivi sasa na maafisa wa TRA wanafanya hivyo with impunity wakijua hawawezi kuchukuliwa hatua kutokana na kufanya uonevu huo. Mh. Waziri; fanya uchunguzi kidogo tu na utajionea mwenyewe ni wafanyabiashara wangapi wameacha kufanya biashara nchi hii kipindi cha miaka mitatu iliyopita na kati yao ni wangapi ambao hawakuguswa na kadhia hii ya kulazimishwa kufanya objection kwa kulipa theluthi moja ya incorrect and unrealistic tax demands.

3. Nchi hii sasa hivi inakabiliwa na uhaba mkubwa wa skilled labour hasa kwenye kazi zinazohusiana na masuala ya business na financial management, IT na hata kwenye elimu. Mh. Waziri, wahitimu wa vyuo vyetu hawana competence inayohitajika na labour market. Ruhusuni sekta binafsi kuajiri watu inaoona ni competent mahali popote (japo utaratibu mzuri uwekwe ili kuzuia watu wasiostahili kupewa vibali). Hatua hii itawezesha skills transfer kuja nchini.

Mh. Waziri, maoni yangu yamelenga kusaidia sekta binafsi ambayo ni mdau muhimu kwa maendeleo ya nchi hii.
Yangu ni hayo kwa leo.
 
Wafanyabiashara wafundishwe matumizi yote ya hizi mashine za efd (kuuza na kununua) kurahisisha kutunza kumbukumbu. Kuacha kufundishwa jinsi ya kurekodi manunuzi ni kuendelea kuweka mazingira ya kuja kukadiriana na maafisa wa TRA kwa kigezo kwamba mfanya biashara ameshindwa kutunza kumbukumbu za manunuzi. Kama mjuavyo risiti za kielectronics hufutika haraka ni vyema elimu ya kuzihifadhi kielectronic ikatolewa.
 
Updates:
Taarifa nilizopata ni kuwa karibu makampuni yote yanayojihusisha na utalii Arusha yamepewa taarifa za kudaiwa malimbikizo ya kodi yasiyokuwa realistic. Kampuni ina mauzo yasiyofika milioni 600 lakini inadaiwa "kodi" ya bilioni na ushee; huu kama sio wendawazimu ni nini?
 
Serikali haina hela kwa sababu imeanzisha miradi mingi mno kiasi kwamba ni lazima kufanya jambo lolote ili hela ipatikane.
NA TUTAMINYWA SANA KWENYE UTAWALA HUU.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali haina hela kwa sababu imeanzisha miradi mingi mno kiasi kwamba ni lazima kufanya jambo lolote ili hela ipatikane.
NA TUTAMINYWA SANA KWENYE UTAWALA HUU.

Sent using Jamii Forums mobile app

Lakini hata mtoto mdogo wa chekechea anajua kuwa mtu hawezi kulipa 100 wakati mfukoni ana 10. Serikali inategemea wafanyabiashara wakope ili kulipia hayo "madeni" ya kodi?
Wasubiri rekodi mpya ya kampuni kufungwa.
 
Makampuni mengi yashaanza kupunguza wafanyakazi wakitumi a kisingizio cha COVID 19 yaliyomo nyuma ya pazia wanayajua wenyewe.

Lakini hata mtoto mdogo wa chekechea anajua kuwa mtu hawezi kulipa 100 wakati mfukoni ana 10. Serikali inategemea wafanyabiashara wakope ili kulipia hayo "madeni" ya kodi?
Wasubiri rekodi mpya ya kampuni kufungwa.
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…