Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Mgonjwa wa moyo wahi THI, upasuaji wa bure...
2008-10-17 10:32:36
Na Richard Makore
Muungano wa nchi za Falme za Kiarabu kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa moyo kutoka nchi mbalimbali duniani leo wanaanza kutoa huduma ya upasuaji wa moyo bure nchini.
Huduma hiyo ya maradhi ya moyo itatolewa katika Taasisi ya Moyo Tanzania (THI) iliyopo jijini Dar es Salaam.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Balozi wa Falme hizo hapa nchini, Mallalla Mubarak, alipozungumza na waandishi wa habari.
Mubarak alisema nchi yake imetoa fedha kwa ajili ya kazi hiyo hivyo matibabu yatatolewa bure THI kuanzia leo.
Alisema Watanzania wote, watoto kwa wakubwa wanakaribishwa katika hospitali hiyo iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa wananchi wengi wanaokabiliwa na maradhi ya moyo wanakufa kutokana na kushindwa kumudu gharama za matibabu nje ya nchi.
Balozi Mubarak alisema wananchi wote wenye matatizo ya moyo wanatakiwa kufika hospitalini hapo ambapo watawakuta madaktari bingwa wakiwasubiri.
Aidha, alisema leo watafanya kazi ya kuwachunguza wagonjwa wote watakaofika hapo na wiki ijayo ndiyo kazi ya upasuaji itaanza.
Alifafanua kuwa madaktari bingwa watakaoshiriki katika upasuaji wanatoka Uingereza, Misri, Ufaransa, India na wengine kutoka hapa nchini.
Aliongeza kuwa utafiti uliofanywa na nchi yake hapa nchini umebaini kuwa watu wengi wana matatizo ya moyo.
Alisema baada ya kumaliza uchunguzi wa awali unaoanza leo, wiki ijayo wataanza kutibu wagonjwa watakaobainika kusumbuliwa na moyo.
Balozi huyo alisema, licha ya mgonjwa kufanyiwa matibabu ya moyo pia atapatiwa dawa zingine bure.
Alisema zoezi hilo pia litafanyika visiwani Zanzibar na Pemba.
Nchi zilizofaidika na ufadhili wa matibabu hayo hadi sasa ni Kenya, Sudan, Ethiopia, Syria na Morocco.
Mkurugenzi wa THI, Dk. Ferdinand Masau, alisema zoezi hilo litachukua wiki mbili na kipindi hicho kila mtu anayesumbuliwa na moyo afike kwa ajili ya kupata matibabu bure.
Dk. Masau alisema watakuwa wanatoa huduma hiyo kwa watu 15 kwa siku wakiwemo watoto na watu wazima.