Kwa wenye uelewa na maswala ya kiuchumi ,Njooni mnisaidie maswali Yangu machache!

King_Villa

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2012
Posts
575
Reaction score
380
Habari wakuu,
Kama kichwa cha habari kilivyosema .
Nina maswali Yangu ambayo naamini wachumi watanijibu kufasaha na nitaelewa !

1. Kwanini bei ya mafuta inapanda na kushuka ikifika mwishoni mwa mwezi ! ? Na Mara nyingi siku za jumatano!

2. Hivi pesa inakuwaje ngumu kupatikana hali tunajua ni makaratasi yaliyochapishwa kwa utashi Fulani ,kwanini serikari isichapishe pesa zaidi afu igawie wananchi wake pesa iongezeke au tatizo nikuwalipa wanaochapisha?

3. Mfano kipindi cha kikwete sukari ilikuwa na bei ya kawaida saivi imepanda maradufu hili tatizo linatokana na nini na hali tunaambiwa uchumi unakua?

4. Nilipopitia stock exchange nyingi naona dollar ya marekani imetawala sana afu bidhaa zao ni chache sana humu nchini ukilinganisha na bidhaa za China ambazo naona yeni iko chini.


5. Hivi serikari kwanini isitumie watu wa masoko kutafuta masoko ya mchicha marekani ili nasisi tuwe tunawapelekea kwenye makontena kama wanavyotuletea magari huku kwetu.

6.Marekani ni nchi yenye pesa na uchumi mzuri sana kwanini haipo katika rank ya nchi tano tajiri duniani .?
 
Namba #2
hapo mi mwenyewe ni swali langu la miaka mingi tu linanisumbuaga i am waiting for answers. Nme subscrible!
 
Kwa uelewa wangu apo namba mbili ni kwamba serikali haiwezi kuprint pesa nyingi na kuziingiza kwenye mzunguko kwa sababu itasababisha mfumuko wa bei... mfano rahisi kila mtu akiwa na fedha nyingi lazima bei za bidhaa na huduma zitapanda.... pesa iliyokwenye mzungunguko lazima iakisi thamani ya bidhaa na huduma zilipo kwenye mzunguko pia.. la sivyo italeta shda.. idd amini alishawai kuchapisha pesa maradufu, balaa lake ni kwamba dhamani ya pesa ilishuka na mfumuko wa bei ulitokea.. kuchapisha fedha pia ina garama zake sio bure
 
Hiyo no sita toa marekabi ni no mbili kwa uchumi imara ikiiongozwa na china
 
Apo namba sita ni ukweli marekani ni nchi kubwa kiuchumi kuliko zote duniani ( kwa kuangalia GDP, pato la taifa).. hii ni kutokana na ukubwa wake kijeografia na idadi kubwa ya watu... ila tukija kwenye pato la mtu mmoja mmoja (per capita income) wapo nyuma
Wachumi wanaangalia ubora wa maisha ya wananchi (living standard) ambayo inapimwa na per capital income. Pato la nchi (GDP)Hua haliangaliwi .
 
Hapo namba tano kwanza ni lazima tukubali bidhaa tunazozalisha sisi bado zipo katika hali duni... hivyo inatuwia vigumu kushindana katika soko la kimataifa
 
Namba moja apo kwenye suala la mafuta kupanda bei kuna umoja wa nchi wanachama wanaozalisha mafuta Hua hao ndo huridhia bei kupanda kilingana na garama za uzalishaji na soko pia.... sina uhakika kama wanakutana kila jumatano ila cha msing tujue izi bei zinapangwa na OPEC
 
Apo namba nne ... dollar kua na supply kubwa imetokana na demand yake ... watu wengi wanaitumia sana kulinganisha na fedha nyingne za kigeni... bidhaa za kichina sawa zipo nyingi ila nazo pia Mara nyingi zinaagizwa kwa dollar kutoka nje... dollar pia ndo tuseme official currency ya dunia
 
Apo namba tatu... bei ya kitu chochote kupanda Hua inachagizwa na sababu nyingi... mfano kukua kwa garama za uendeshaji wa viwanda, hali ya hewa , hali ya kisiasa n.k ... hizi factor zote lazima uzicheki pia
 
#1.Bei ya bidhaa yoyote(sio lazima mafuta) inaweza shuka na kupanda wkt wowote(sio lazima mwisho wa mwezi tu) kutokana na market force(s) DD & SS which determines the price of the commodity.
-Mahitaji ya bidhaa (Demand) yakiwa makubwa kuliko uzalishaji/upatikanaji (supply ) lazima bei ipande(price increase) and vice versa is true.
-Wkt mwingine kuna kuwa na regulatory bodies kwenye inchi (mfano EWURA kwa hapa Tz) kwa case yako ya mafuta ambayo inasaidia kubana wafanyabiashara wasipandishe bei wanavyotaka,bali bei ziendane na soko la upatikanaji wa bidhaa husika duniani /kwenye mzunguko.
-Ewura ndo wenye mamlaka ya kuratibu bei na huwa wanafanya hivyo kila mwanzo wa mwezi kulingana na sababu nilizotaja hapo juu.
 
#1 kwa uelewa wangu, nadhan ni utaratibu waliojiwekea nchi zinazolisha mafuta kwa wingi kureview bei za uzalishaji kila jumatano ya mwanzo wa mwezi na pia kuangalia mwenendo wa soko la bidhaa husika...
 
#2 Pesa zikichapishwa kwa wingi thaman yake huwa inashuka na kusababisha mfumuko wa bei ambao unamlazimu mnunuzi kubeba mihela mingi kwa ajili ya kununua bidhaa anzozihitaji.
 
#3 uadim wa sukar unaosababishwa na uzalishaji mdogo wa viwanda vya ndani na na marufuku iliyowekwa kwenye kuingiza bidhaa hiyo... ni moja ya sababu ya sukar kuwa bei juu kulinganisha na kipindi cha JK
 
#2 kama hela ikichapishwa kwa wingi ikawepo mtaani uzalishaji utapungua kwa kasi kubwa hakuna atayetaka kufanya kazi ngumu angali pesa anazo
 
#2 Pesa zikichapishwa kwa wingi thaman yake huwa inashuka na kusababisha mfumuko wa bei ambao unamlazimu mnunuzi kubeba mihela mingi kwa ajili ya kununua bidhaa anzozihitaji.
Swali la ufahamu kwani pesa inachapishwa au inatengenezwa na nini? I mean ni material gani inayobeba asilimia kubwa ya pesa (noti) inayotengenezwa?
Halafu kwa mfano serikali sasa hivi inasumbuka na sijui kununua ndege, kujenga reli ya standard gauge na mpaka inaenda kukopa fedha nje swali kwanini isichapishe hela hizo kisha kufanyia hiyo miradi (naimani jawabu hapa halitakua mfumko wa bei)
 
Najibu namba tatu.....
Huwa tunaambiwa uchumi unakuwa kwa kuongopewa sababu wanajua kuwa watz sio watu wanaopenda fiatilia habari, ila udaku,... Ndio maana ni rahisi kumdanganya mtanzania kuwa uchumi unakuwa at the same time anaona ugumu wa maisha na anaishia kukubali..
 
haha naona umemwaga notes
Kasema hajui masuala ya kiuchumi layman language ilihitajika acha kukariri notes
 
Hata mimi hapo bado sijaelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…