Kwa wenye uzoefu na NMB

Manselly

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2010
Posts
456
Reaction score
130
salaaaam.
Jamani mimi ni mtumishi wa serikali Tamisemi. Nina kama mwaka mmoja na nusu sasa tangu nimeanza kazi na sijawahi chukua mkopo mahali popote.
Naomba wanao fahamu, je naweza patiwa mkopo na NMB manake nina barua ya kupangiwa kituo cha kazi tu ila ya kuthibitishwa kazini bado sijafatilia pia bado sijapata tsd namba ila salary slip inasoma vizuri tu na ninazo zote pia kitambulisho cha kazi ninacho.
Naomba wanaojua je ni lazima nifatilie tsd namba na letter of confirmation au naweza pata mkopo bila ivo vitu
 
Nenda tawi lolote la NMB karb nawe watakusaidia huchukui muda ni kitendo cha dakika 3
 
naelewa mkuu lakini najua humu wapo wazoefu waliowahi kukopa. Hapa jirani kwangu hakuna nmb mpaka wilayani ndo mana nimeuliza pengne nmb wapo humu
 
We ni mtendaji wa kijiji au kata?
Huwezi kupata mkopo bila comfirmation letter. Your employment status is still in probation period, wait untill you get a full recognition. Na utwambie unachukua mkopo what for? U wanna buy a motorcycle/car and for which purpose?
Kopa kwa sababu maalum hasa biashara uliyokwisha fanyia upembuzi yakinifu.
Otherwise unajitengenezea ugumu wa maisha pasipokujua.
 
kwa uzoefu wangu mimi mkopo utapata, mana wanachohitaji sana sana ni kitambulisho na salary slip na barua kutoka kwa mwajiri wako ambae ndo mdhaminii wako basi
 
Mkuu mrsleo hiyo barua kwa mwajiri ndio tatizo kama hujapata comfirmation.
Unless acollude na huyo mwajiri which is illegal and leading to direct shortaning/reduction of the granted loan as compansation.
 
Last edited by a moderator:

haya mkuu nimekupata pia nashukuru kwa angalizo niko makini sana sana ndo mana nina zaidi ya mwaka na nusu kazini sijawahi kukopa na sasa ndo muda muafaka maana tayari najielewa. Kuna biashara fulani nataka kufanya ambayo nilishawahi kuifanya nikaona inanilipa sana
 
Ila jaribu kwenda benk watakupatia maelezo ya uhakika..mm niliwah kupatiwa mkopo kwa kuambatanisha vifuatavyo:-barua ya kupangiwa kituo, salary slip mbili za miez ya karibu , kitambulisho cha kura... barua ya utambulisho kutoka kwa muajiri wangu pamoja ya fom ya mkopo niliyojaza na nikapatiwa mkopo.
 
safi sana wakuu shukrani sana acha nijitahidi nifike eneo husika kama watakomaa mpaka barua ya kuthibitishwa poa itanilazimu kuanza kuifatilia sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…