Kwa wenye uzoefu naomba ushauri kuhusu biashara ya uwakala wa miamala ya simu

Mazima1

Senior Member
Joined
Dec 31, 2020
Posts
192
Reaction score
550
Habari wakuu,wiki kadhaa zilizopita nilipost uzi nikieleza Nia yangu ya ya kuanza biashara ya uwakala wa miamala kwa Mtaji wa 2.5M, nashukuru kwa maelekezo mliyonipa,

Leo narudi Tena kuomba ushauri na muongozo kutoka kwa wale ambao mlishawahi kufanya biashara hii, Je ni mambo gani nizingatie?mnakabiliana vipi na matapeli? Pia kama Kuna lolote ambalo unahisi ukinishauri litanifaa naomba unishauri

Very soon naanza utekelezaji wa wazo langu
 
Jiandae kwa yote mkuu. Ila km unajiamini usikate tamaa ndio kujifunza,kisichokuua kinakukomaza kiaskari.
 
Pambana mkuu usikatishwe tamaa na baadhi ya maoni ya wadau, hamna biashara isiyokuwa na changamoto.
 
Wengi wanasema imesha kua biashara kichaa kwakua mawakala wamekua wengi location Ni zile zile. Ukiotea location utaenjoy mkuu.

Kihusu utapel Kuna usemi hua tunasema lazima ukaribishwe mkuu hii haikwepeki cha msingi Kama unataka kuepuka au kupunguza mazingira ya kutapeliwa epuka kutumia simu au lain ya kazi kuwasiliana na watu au wateja wako.

Epuka, epuka, narudia Tena mala ya tatu epuka kumpa mteja simu ya kazi ajaze namba katakata karatasi mteja aandike namba Kama hajui Ni Bora akutajie kabla ya kuthibitisha utamuuliza jina Kuhakiki.

Matapel wengi wanakuja wanavunga Kama wanaongea ma sim Kisha anaomba simu aandike namba hapa Ni kosa kubwa.
 
Sawa mkuu
 
Back
Top Bottom