Kwa wenye uzoefu, tupeane dondoo za biashara ya kuuza saruji (cement) kwa rejareja

Kwa wenye uzoefu, tupeane dondoo za biashara ya kuuza saruji (cement) kwa rejareja

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
19,582
Reaction score
14,167
Habari wadau, kazi iendelee

Kwa wale wenye uzoefu wa biashara ya simenti tupeni dondoo Kwa maana ya faida, changamoto na namna ya upatikanaji.

Hii ni moja ya biashara nayopenda kuifanya japo baada ya kuuliza hapa na pale,kuna jamaa alisema eti Ili uone faida yake ni nzuri mtu akianza na mzigo wa Tani 60 yaani mifuko 1,200 sawa na semi 2.

Sasa baada ya kuchakata nikaona hapo si chini ya mtaji wa mil. 20.

Kwa wazoefu hivi haiwezekani kuanza na wastani wa mil.10 yaani Tani 30 ila niwe na vijiwe 2? Ushauri tafadhari.
 
Utokaji wake unategemea na sehemu biashara ilipo. Ikiwa ni maeneo ambayo yameendelea tayari mzigo utakuwa hauendi Sana mfano Duka liwe Mikocheni Ila Duka likiwa kisemvule, chamazi mzigo utatoka sana.

Unaweza kuanza na gari moja Ila nakushauri usiuze cement yenyewe weka na bidhaa nyingine za ujenzi maana hapo utakuwa unatumia njia ndefu kupata faida kidogo. Mfuko Kwa reja reja ni Kati ya 1000 Hadi 1500 angalia na gharama zake za uendeshaji..
 
Mkuu ulipo sema ninanukuu (Mfuko Kwa reja reja ni Kati ya 1000 Hadi 1500 ) Je umekusudia kila mfuko hiyo ndio faida yake?au ndio bei ya uuzwaji wake kila mfuko wa simenti?
 
Back
Top Bottom