Kwa wenye uzoefu wa kuagiza Magari kutoka Japan

ukisoma maelezo ya tradecarview yanajieleza wazi umuhimu wa kutumia paytrade katika kufanya malipo ili kuwa na uhakika wa usalama wa manunuzi.na wanasema wazi kuwa ukitumia paytrade na usipoletewa gari unarudishiwa pesa zako.sasa tatizo letu watanzania wengi hatupendi kusoma maekezo kwa umakini na pia tunapenda sana kukwepa gharama.na kulipia gari kupitia pattrade kuna gharama na sie tunapenda kukwepa hiyo gharama bila kujua tunajichimbia shimo.mhusika pole sana.na kwa yule aliyeona wazi wamekata gharama za paytrade hii inatokana na pale unapoanzq kubargain jamaa wanakuwaga wajanja wanaondoa kwanza paytrade,ukikubali imekula kwako.haimaanishi tusi bargain ila tu bargain tukihakikisha huondolewi kulipa kwa paytrade maana ndio hakikisho pekee la kulipa na kuletewa gari.
 
BE FORWARD forever, sihami ng'o japokua na wenyewe wanadelay sana kudeliver items zao kwenye final destination lakini huduma yao ya uhakika.
 
Good news
 
Kiongozi vipi ulifanikiwa kupata gari yako?
 
Mkuu claim yako imeishiaje na hao jamaa
 
Ni bora kununualia hapa hapa bongo kwenye hizo showroom zao

Pole sana....showroom za bongo magumashi mengi na wanainflate bei sana....achilia mbali kuchomoa injini nk....woga ndiyo chanzo cha wengi kununulia magari kwa matapeli wenye showroom
 
Tayari mkuu nilishafanikiwa kitaaambo... Reg yake ni #T_401_DCN
Hongera sana, sasa nataka niagize nipe utaratibu wa kuagiza kwa malipo ya pay trade, maana proforma invoice pamoja na invoice sijaona hiko kipengele, n kupitia mtandao wa cartrade view kwa kampuni ya Real Motor Japan
 
www.tradecarviews.com/jp ndo website niliyotumia kununua gari tena kwa sellers hao hao #Real_Motor_Japan . Kama unataka kununua kwanza inatakiwa u create account au sign up kene iyo website ya tradecarview, kisha unaingia kene kuchagua mikoko tofauti tofauti unayotaka. Kabla hujafanya submission ya gari hakikisha umeisoma vzr Displacement zake, umri wa gari na mengine kibao mpka uridhike nayo kisha unaisend kwa sellers, then subiria akiipata msg yako mnafanya negotiations naye kwenye iyo iyo website, ucjaribu kumpea email address yako nje na tradecarview. Hakikisha mawasiliano yote yanafanyika kwenye iyo website na c vinginevo. Kama mtakubaliana basi yeye atakutumia profoma invoice kisha utai download kwa ajili ya kufanyia payment. Malipo huwa yanafanyika kwa njia ya Telegraphic Transfer T/T. Kama kuna sehemu hujanielewa niambie nikupe maelezo kwa mapana....
 
hayo yote nimeshayafanya nipo kwenye invoice payment, tatizo wakat najaza proforma sijaona sehemu ya opt kutumia pay trade, ila invoice ina account ya trade car view, ss ishu inakuja mbona gharama za pay trade sijaainishiwa na pay trade hulipwa muda gani pamoja na invoice kwenye CIF au separate
 
Invoice huwa inakuja na opt mbili, ya kwanza ni kuisubmit pacpo paytrade...
Ya pili inakuwaga with paytrade service....
Gharama huwa inajumlishwa yote humo humo. Maana kene negotiations list kule ndo mtakubaliana bei full pamoja na huduma zingine.
Inawezekana ikawa sahv paytrade service inatolewa bure ndo maana hujaona opt iyo. Nilipata email moja wananambia kuwa now paytrade service is free.. Inawezekana ishaanza kufanya kazi.
Ukiona inazingua unaweza nunua pacpo hata kutumia paytrade ilimradi tyu makubaliano yamefanyika ndani ya database ya tradecarview website... Hiyo invoice utayotumiwa ndo itakupa kila kitu hadi bank information .
 
Watakuwa wamefuta basi maana makubaliano tumefanya kwenye website ya tradecar view na account ni ya tradecar view
 
Watakuwa wamefuta basi maana makubaliano tumefanya kwenye website ya tradecar view na account ni ya tradecar view

Haina tatizo, we fuata procedures zote kila kitu kitaenda sawa. Utapotumiwa bank details kwa ajili ya kukamilisha payment hapo ndo pressure zaidi make wanakaa cku tatu au nne ndo utatumiwa message ya alert reflection kuwa payment approved! You wait for the copy of Bill of Lading, shipment schedules zote!
 
Hivi kwa mfano nikiingizia bandari ya Mombasa...lazima nilipe kodi ya Tz....Nisaidieni jamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…