Kwa Weusi, Jux na Vanessa: Hip hop na R&b kutoboa inawezekana, ila Afrika ni ngumu sana

MARA IMARA

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2015
Posts
238
Reaction score
163
Nimeanza kuona weusi na Vanessa wanatumia resources kibao kujitangaza AFRICA ila mimi kwa mtazamo wangu naona ni ngumu. MOJA YA SIFA YA MALENGO NI KUWA Lazima yawe ACHIRVABLE( yawe yanatimilika) wawe makini wanaweza tumia mtonyo kibao wakaishia patupu

v Yawezekana hawa jamaa wa WEUSI, na VANESSA wana malengo mazuri sana ya kujulikana kimataifa ambapo itawasaidia kupiga hela na kuitangaza bongo lakini ukweli utabaki pale pale HIP HOP na R&B haziwezi kutoboa mipaka si kwa wasniii wa bongo tu : mimi nimekuwa hadi hapa nilipo sijawai ona msanii wa hip hop au R&B akitusua Africa nzima hadi nje, wapo waliojaribu kwa R&B km akina 2face lakini kwa HIP HOP ni ngumu sana,ili kutoboa lazima uje na mziki wenye midundo tofauti ; angalia wasnii waliotoboa Africa , akina seif keita,yous ndou, makeba, makoma, wa congo, p square mafiki zorro. Ivon chaka chaka . HAYA NTAJIE WASANII 3 TU WA R& B, HIP HOP waliotusua Africa na ulaya

v Huwezi peleka hip hop na r& b America na ulaya ; muulizeni AY keshafanya weee mambo kibao lakini wapi alipo hata Africa tu haimjui: hata kwa ma black America wenyewe kutoboza wanafanya kazi kweli kweli: na sisi wabongo tunawajua kwa Sababu bado watangazaji na ma DJ wanaona ni ujanja kupiga na kujua nyimbo za nje ndo maana unakuta DJ wanaona bora apige wimbo wa rihanna ambaye yuko hukooooo amarica hajui hata dar es salaam kuliko kupiga nyimbo ya 20%,

v Mziki ni utamaduni na kila nchi inakumbatia wasnii wake hata hao wanaijeria wameshindwa toboa America na ulaya

v Nyimbo km ya navy kenzo ile ya game inaweza toboza, ndo maana mtu kama saida karoli, mr nice, diamond kiaina wameweza
v Huyo dogo niki wa pili ana PHD BADALA KUUMIZA KICHWA JINSI GANI WANAWEZA KUTUMIA SOKO LA BONGO AMBALO BADO HATA ROBO HAWAJALITUMIA KUPIGA HELA wao wanataka kukomaa eti watusue Africa kwa HIP HOP?
 
Tumeazima Rap na RnB kutoka America. Kujaribu kukubalika kwao kwa mahadhi hayo, ni sawa na mtu aje na kujaribu kukuchekesha kwa joke uliyoitunga mwenyewe.

Sarkodie alijaribu kwenda ki-Africa, ila nae siku hizi naona anafanya yale yale.
 
Tumeazima Rap na RnB kutoka America. Kujaribu kukubalika kwao kwa mahadhi hayo, ni sawa na mtu aje na kujaribu kukuchekesha kwa joke uliyoitunga mwenyewe.

Sarkodie alijaribu kwenda ki-Africa, ila nae siku hizi naona anafanya yale yale.

Umemaliza mkuu, anyway kumbe kiswahili unakimanya teh!
 
Mbona akina cassper nyovest, mrcashtime na aka wametoboa tu kwa hip hop na rapper phyno pia cha msingi hapa tufanye midification ya hip hop yenye vionjo vya kiafrica tusikate tamaa
 
Usijifunze sana kwa waliofeli, usiseme haiwezekani wakati hujajaribu,'Nusunusu' ya johmakin imeshafika no.1kwenye chart za channel O, dalili njema...GO ON WEUSI
 
Hahahaha.....vaa miwani miwani ukiona.......!weusi hatua kwereeee u just go....get
 
What if wao wakiwa wa kwanza kutoboa huko unakodhani ni ngumu? Hakuna kinachoshindikana chini ya jua mkuu. Anyway ushauri wako unasound ila kwa mbaaaaali naona vielement vya wivu..
 
Kwanini hawatusui? ngoja nikupe darasa kidogo Hip Hop ya Afrika wanadhani ni midundo bila kujali ni nini unachoimba na lyrics zako.

America wako vizuri sana kwenye uandishi sie bado ukisikia mistari ya mtu kama AKA, SARKODIE sijui ICE PRINCE kiukweli ni ya kitoto kama mtu umezoea kuwasikiliza kina drake, kendrick, yelawolf, big krit, tech n nine e.c.t.

Producers pia wanachangia eti mtu kama nahreel atengeneze mdundo ambao utashindana na watu kama kina just blaze, bangladesh, pollow da don, alchemist ni kitu ambacho hakipo.

Pia sie hatuna origin yetu ya music bado hatuna ladha ya music ya kwetu tunatakiwa tuwe na kitu chetu wenyewe ndio maana mdogo mdogo, ya diamond naikubali ile ndio style yetu ya music tuwekeze kwenye mduara.

Kingine ni ulimbukeni wa ma-dj wa bongo hawajui mziki wa nje..
 
A.K.A, Sarkodie, Casper nyovest

hao mnawajua nyie ambao mnafatilia lakini ukiuuliza kati ya watu kumi kwa kila nchi kenya , uganda na tanzania mtu mmoja kati ya kumi ndo na anaweza kuwa anawajua .
 
What if wao wakiwa wa kwanza kutoboa huko unakodhani ni ngumu? Hakuna kinachoshindikana chini ya jua mkuu. Anyway ushauri wako unasound ila kwa mbaaaaali naona vielement vya wivu..

sijasema haiwezekani ila ni ngumu sana sana na lazima walinganishe gharama na faida: kutumia millioni 50 kutengeneza video eti kisa ipigwe tu MTV wakati baada ya hapo hupati shows za maana nje ni ujinga.. kama wanataka ummarufu watapata lakini lazima waangalie italipa. wasanii wengi bomgo wanapenda umaarufu sio hela
 
Usijifunze sana kwa waliofeli, usiseme haiwezekani wakati hujajaribu,'Nusunusu' ya johmakin imeshafika no.1kwenye chart za channel O, dalili njema...GO ON WEUSI

kupigwa kwa video kwenye channel o wakati hamna return ni kuinufaisha tv station
: joh kapiga show ngapi nje zaidi ya coke studio?:
 
hao mnawajua nyie ambao mnafatilia lakini ukiuuliza kati ya watu kumi kwa kila nchi kenya , uganda na tanzania mtu mmoja kati ya kumi ndo na anaweza kuwa anawajua .

Huwezi ukawajua wachezaji wa rugby kama hufatilii rugby. Mtu hadi anakua nominated B.E.T na bado unasema ngumu kutoboa kwa Hip hop, serious?
 
Huwezi ukawajua wachezaji wa rugby kama hufatilii rugby. Mtu hadi anakua nominated B.E.T na bado unasema ngumu kutoboa kwa Hip hop, serious?

Alichoongea jamaa ni kweli kabisa, hao wakina A.K.A, Sarkodie wataishia kupata umaarufu wakuwa nominated kwenye tuzo kubwa lakini hawawezi kuwa sawa na wasanii wanaoimba muziki wa kiafrica kama Fally Ipupa,Davido, Wizkid, Mafikizolo, Psquare, etc. Hao wamepiga shows nyingi sana Africa, ni ngumu hao wa Hip hop kupata shows nchi nyingi tofauti kama hao niliowataja
 
Hip hop haipo katika mahadhi ya kuchanganyika sana kama genre zingine za music. Hip hop kama hip hop lyrics comes first before melody hivyo, kwa mfano, Roma akiimba kuhusu CCM au matatizo yetu yakibongo hata kama mtu anaelewa kiswahili Cameron Bado anakua nje ya walengwa wa wimbo husika.

Hao kina sarkodie, AKA, ice prince me nawaiata wasanii wa YouTube watu wanaowafahamu ni watu ambao wanajihusisha na burudani kila siku yani unatumia nguvu nyingi hadi kuwajua wakati Dayamondi au davido hata usipotaka kuwajua utawajua tu

Iko wazi kutoboa kupitia hip hop Ni ngumu sana, ila acha waendelee kujaribu we'll never know how far we can go kama hatutojaribu kabisa
 
Kweli hip hop ya Afrika ni ngumu kutoboa nje ya mipaka. Weusi watatoka endapo watafanya haya pia
1.Kutumia mdundo(beats) kali za kuchezeka ( Watu wanapenda kuparty zaidi , hawaitaji meseji)
2.Wa-switch flow kutengeneza melody tamu
3.Midundo ya asili ya kiafrika watumie sana kwenye nyimbo zao
4.Waendelee kutoa video kali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…