Kwa yale maisha ya kupigana na kukashifiana, maoni tafadhali

Kwa yale maisha ya kupigana na kukashifiana, maoni tafadhali

1.Hakuna tabia chafu na ya kishamba kama kupigana. Haisadiii kabisa.(HAPA HAIWAHUSU WALE WA MUSOMA)2.Sijawahi kunyanua mkono kumpiga mwanamke yeyote.3.Ukikaa na mpenzi wako...na taratibu na kwa upendo mkuu umweleze kakosea wapi itamuuma sana,hiyo ni zaidi ya FIMBO MIA. ............WENYE TABIA HII IACHENI MARA MOJA( UKIONDOA WATU WA MKOA WA MARA)
Hongera sana.endellea na moyo huo
 
kwa kweli ni k2 cha ajabu sana kuona mambo kama hayo yanatokea zaidi inauma pale unapokuta mwanamke au mwanaume kasoma lakini ustaharabu o kabisa fikiria una gf wako mmeanza tu urafiki wakawaida mara unagundua tabia ya mwenzako na unamwambia yy anakuwa mbogo ustaharabu unakwisha matuc yanaanza, kejeli, unaanza kusemwa kila mahali nakujitapa uwezi kuniaacha marafiki zangu nilishawaambia.nafikiri kama watu wakiamua kukubali ukweli na kuyasawazisha wenyewe na kuyaeshimu maamuzi yao wenyewe shida zingekwisha kabisa
Hata me nafikiri ustaarabu ni kitu cha bure kabisa.haina haja ya kugombana wala nin.umegundua hamuwezi kwenda njia moja mnaachana kistaarabu kabisa.embu fikiria mwanaume mnaanzisha mahusiano mnaenda mpaka kwa wazazi na kumaliza,after kuanza kuishi unagundua kumbe umeingia chaka.tabia sizo.magonjwa mengi siku hizi unaamua tena mapema tu kuwa ni bora kila mtu akfata njia yake ss linapokuja swala la nirushie vyangu there a problem starts.mlolongo wa sababu.kwann usiwe msaarabu ukarudisha kisichokuwa chako?mali ina thamani ikiwa yako.vya dhuluma haviliki.hata ukifanikiwa kumeza ipo siku utavitapika tu
 
Tembeza kichapo havi pambaf.................ujinga apeleke kwao !!!!!!!!!!!!!:sick:
 
Kupigana,kukashifiana,kudharauliana,kutoheshimiana,
kote ni tabia mbaya kwa wanandoa au wapenzi.
Hayo yote yanatokea kutokana na kukosekana kwa hekima na busara,
kutoweza kuwa na uwezo wa kudhibiti hasira pindi zinampanda mtu,
kuchukua maamuzi ya haraka pindi anapokwazwa na mke/mume,mpenzi wake.

Kutosema vipigo unavyopewa na mtu wako wa karibu,
kunatokana woga kuwa ikiwa nimesema je jamii itanichukuliaje?,
na hii inatokana na malezi tuliyopewa/tuliyokulia kutokuwa na uwazi juu,
ya kinachoendelea katika familia zetu. Baadhi wamekuwa na kuonawaona,
mama zetu wakipigwa mpaka kufikia hatua ya kupata ulemavu mwilini,
lakin bado hawakudiriki kusema wazi waliendelea kuvumilia ndoani kutulea,
na kufikia hatua ya kutenganishwa na vifo katika ndoa zao.

Suluhisho la tatizo hili ni sisi wenyewe kufahamu kuwa tunaokuwa nao,
katika mahusiano yetu siyo malaika bali ni binadamu wenzetu wanaoweza,
kutufurahisha na kutuudhi kwa namna moja au nyingine. Tunapoudhiwa,
na wapendwa wetu basi tuweze kudhibiti hasira zetu,hekima na busara
zitumike zaidi katika maamuzi yetu, tusipende kuchukua maamuzi ya haraka,
tusiruhusu hasira zitutawale bali tuzitawale. Tuvunje ukimya pale inapowezekana/inapolazimu tu, lakin
siyo kila jambo/tendo tunatakiwa tuvunje ukimya(ukimya wakati mwingine una faida)
LA KUZINGATIA ZAIDI tusiruhusu/tusisababishe kufanyiwa huo ukatili. HIZO SABABU ZA KUPIGWA
KWETU TUJARIBU KUZIONDOA, tusiwe wepesi wa kulaumu kupigwa kwetu tu pasipo sisi wenyewe,
kujichunguza kwanini tunapigwa/ dharauliwa. TUWE WEPESI WA KUJIKOSOA KABLA YA KUKOSOA WENGINE.
 
Hata me nafikiri ustaarabu ni kitu cha bure kabisa.haina haja ya kugombana wala nin.umegundua hamuwezi kwenda njia moja mnaachana kistaarabu kabisa.embu fikiria mwanaume mnaanzisha mahusiano mnaenda mpaka kwa wazazi na kumaliza,after kuanza kuishi unagundua kumbe umeingia chaka.tabia sizo.magonjwa mengi siku hizi unaamua tena mapema tu kuwa ni bora kila mtu akfata njia yake ss linapokuja swala la nirushie vyangu there a problem starts.mlolongo wa sababu.kwann usiwe msaarabu ukarudisha kisichokuwa chako?mali ina thamani ikiwa yako.vya dhuluma haviliki.hata ukifanikiwa kumeza ipo siku utavitapika tu
kwakweli ukijua ustaarabu ni k2 cha bure wala shida isingekuwepo kabisa kupita pitapita kwa wa2 wasiohusika mlipoanzishana kuwahusisha wazazi ndugu watumishi kutangaza kila mahali kwenye jf kutumia w2 msg kupigia w2 cm wakati ata kuchumbiwa bado atakumbulishwa rasmi bado atapale unapomlazimisha mwanaume akajitambulishe kwenu akikataa sio mwanzo wakuanza kumfananisha na wanaume walokutosa baada ya kuwatamkia ivyo uwezi kumwambia mwanaume ata fulani na fulani na fulani walifanye ivi ivi ila niliwapelekea timbwilitimbili la kufa m2 awatanisahau alafu unaanza kumtisha mwanaume ucponioa utaona nitahakikisha na kuaibisha kila mahali mpaka dunia wajue
 
[/COLOR]Mkuu hapo kwenye red inamaana hao watuhawahusiki na huu ushauri wako[/B]
ha ha ha ha, watu wa musoma kudundana ni moja ya dalilli nzuri kuwa KUNA PENZI lina exist kati yao,kwa uelewa wangu. Wenyewe hawajabisha wewe mkuu unataka details????!!!!!!!!
 
kwakweli ukijua ustaarabu ni k2 cha bure wala shida isingekuwepo kabisa kupita pitapita kwa wa2 wasiohusika mlipoanzishana kuwahusisha wazazi ndugu watumishi kutangaza kila mahali kwenye jf kutumia w2 msg kupigia w2 cm wakati ata kuchumbiwa bado atakumbulishwa rasmi bado atapale unapomlazimisha mwanaume akajitambulishe kwenu akikataa sio mwanzo wakuanza kumfananisha na wanaume walokutosa baada ya kuwatamkia ivyo uwezi kumwambia mwanaume ata fulani na fulani na fulani walifanye ivi ivi ila niliwapelekea timbwilitimbili la kufa m2 awatanisahau alafu unaanza kumtisha mwanaume ucponioa utaona nitahakikisha na kuaibisha kila mahali mpaka dunia wajue
Me sidhan kama kuna mtu anaweza akalazimisha ndoa.tena na mtu kimeo.amae ameundergo bankruptcy sababu ya upuuzi.me nafikiri its a way ya kujitetea usilipe unavyodaiwa
 
Hivi kwaa nini inakuwa hivi? Inakuwaje watu wanaopendana wanapigana? ...Umewahi kupigwa au kumpiga, kumkashifu na kumtisha mwenza wako?....unadhani ni vema kufanya hivyo?....Ukiacha kupigana na kutishiana, ni njia gani zingine zaweza kutumika kuresolve issues za mahusiano? Ukijikuta uko kwenye uhusiano au ndoa yenye domestic violence utachukua hatua gani? Je unaweza kuongea na kushare na marafiki zako au jamaa zako masahibu yanayokukuta? Ni jinsi gani tunaweza kuzuia domestic violence?

Mimi nashangaa sana watu ambao bado wanakumbatia suala hili la kijinga. Mimi binafsi sijawahi na sitegemei kumpiga, kukashifu au kumtishia mwenza. Naamini sio vyema kwani tutakuwa tunafundisha tabia mbaya watoto wetu. Nakubali kuna bump huwa zinatokea lakini kuna njia nyingi za kusolve. Kikubwa ni kukubali ya kwamba mwenzangu ni binadamu kama mimi na pia anatoka kwenye background tofauti na mimi. Na sitegemei yeye kufanya 100% ya kile mimi nataka. Hapo utaona ku-accept limitations ndani ya mahusiano ni njia mojawapo ya kuovercome na kutatua mambo mengi.

Mimi nadhani domestic violence inasababishwa na (1) Kutojiamini kwa mwanaume na kutaka Power kwa lazima. (2) Maisha ya nyuma ya wanandoa au marafiki na (3) makubaliano ya mahusiano ya baadaye ya wanandoa au marafiki. Hapa utaona wengine wanakubali kupigwa kwa sababu mbalimbali. Kukubali sio lazima uandike kwenye karatasi. Ukikaa kimya umekubali.

Kabla watu hawajawa marafiki wanatoka kwenye mazingira tofauti. Kuna wale wanaotoka kwenye familia zilizowafundisha kuthamini wengine hasa wanawake, mara nyingi hawa wanafundishwa kukubali kosa, kukubali mapungufu na kuomba msamaha. Pia kuna wale ambao wanatoka kwenye mila zinazothamini mwanaume zaidi. Mara nyingi mila na tamaduni hizi zinachangia kwa nguvu kwa wanaume kunyanyasa mwanawake. Kwenye familia za tamaduni hizi ..mwanaume anatafuta kuonyesha power yake kwa kupiga na kunyanyasa familia. Sometime..inaenda hadi kwa watoto..yaani utakuta baba akiingia watoto wanakimbilia chumbani..kwani kipigo kinaanza kwa mama na kumalizikia kwao..Mimi naona watu wenye kufikiri hivi wamekosa self confidence kutokana na maisha na tamaduni wanazoishi.

Pia tukumbuke kuna asilimia ndogo ya kukosa confidence ambayo inatokana na mmoja wenu kuji-feel anamakosa na hivyo kuficha makosa yake.. “Guilty Consciousness” Hapa mmoja wa wanandoa/partner ana-cheat hivyo na anakosa confidence nyumbani na hivyo dhamira ndani ya moyo inamsuta daima. Kufidia pengo hili anakuwa mbogo kwa mwenzake.

Tabia za kupiga wapenzi zimepitwa na wakati, ni za kipuuzi na kijinga. Ili zifutike, kikubwa ni mawasiliano kabla na baada ya mahusiano. Mawasiliano ni issue muhimu…Mwanamke na Mwanaume inabidi muambiane frankly ni nini unataka na nini hutaki na pia uko tayari kupoteza hilo penzi au ndoa.

Kama utajikuta umeingia kwenye domestic violence..inabidi utoke haraka sana. Kwa thamani yeyote ile hata kama kuvunja uhusiano.
Kama kupigana kunatokana na tabia za kilevi.. wote muwe wazi.. Mtu akikugusa umwambie kwa uwazi..hakuna cha kusema mmoja avumilie kwa sababu za kiimani.. kumbuka Mungu hapendi violence.. na Mungu hapendi wazazi wafundishe watoto violence, hivyo hakuna kupatanishwa na wazee kwa maneno eti kaa ulee watoto wakati huyo baba anafundisha watoto tabia mbaya..mkishindwa kuyatatua na kubadilika vyombo vya dola viko wazi..weka mtu ndani.. anza maisha mapya..take custody ya watoto..kwani hata hakimu hawezi kukubali kumpa watoto mlevi au mtu mwenye tabia za kilevi kupiga ovyo.

Mimi binafsi sioni sababu ya watu kushare na wengine masahibu yao kwani lazima wayamalize wao mwenyewe! Full stop! Ila wanaweza kushare na wengine outcome zilizotokana na jinsi walivyomaliza masahibu hayo..Kama vile kwanini wameamua ku-divorce, au kwanini ameamua kumpeleka mke au mume polisi..au rumande segerea.

With millions of apologies for a long comment. But I thought, it worth to open up my chest.
 
Back
Top Bottom