Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 25,968
- 36,044
Usiku wa pambano kati ya Juma Choki na Tony Rashid uligubikwa na malalamiko kila kona kulingana na aina ya maamuzi waliyotoa majaji.
Miongoni mwa mapambano ambayo maamuzi yake yalileta utata ni haya
1) Debora Mwenda vs Dorothea.
2)Dulla Mbabe vs Hussein Itaba.
3) Main card (Juma Choki vs Tony Rashid).
Kwa upande wa Debora ameenda mbali zaidi na kutishia kutocheza tena mapambano yatakayofanyika hapa TZ kulingana na hujuma alizofanyiwa.
Lalamiko lake kuu ni kwamba miongoni mwa majaji , mmoja wapo alikuwa ni kocha wa mpinzani wake hivyo ndio maana alinyimwa ushindi wa wazi ambao kila mmoja alishuhudia.
Pambano lingine lililozua utata , ni hili la Itaba na Dulla Mbabe.
Wengi wameshangazwa na maamuzi ya sare waliyotoa majaji, wengi wanadai Itaba ameshinda hilo pambano.
Wengi wamempa Itaba ushindi kwa sababu alim knockdown Dulla Mbabe mara 3 katika round tofauti , japo kiuhalisia alim knockdown mara 2 pekee ile ya tatu alimkwaa haikuwa knockdown.
Pia hata ingekuwa knockdown hii sio sababu ya bondia kuwa mshindi .
Kwa utaratibu wa miaka ya nyuma 3 knockdowns kwenye round hiyo hiyo moja ilihesabika kama knockout na referee ana haki ya kumaliza pambano , hii sheria hata hivyo ilishafutwa kitambo .
Dulla Mbabe alimuangusha Itaba mara 1 lakini ame score sana kuliko Itaba na kiuhalisia Dulla Mbabe ndiye alipaswa kuwa mshindi na sio huyo Itaba.
Kwa main card napo utata kila kona.
Kiuhalisia Tony ilipaswa atangazwe mshindi na sio Choki.
Choki hakuweza kabisa kufungua gadi ya Tony na ngumi zake hazikuonekana kuwa na madhara yoyote kwa mpinzani wake.
Mbali na haya , yapo mapambano mengine ambayo nayo mara kwa mara yamekuwa yakileta malalamiko kwa mashabiki kulingana na maamuzi yaliyotolewa .
Sasa hii hali kadri inavyozidi kuendelea ndivyo inapoteza hamasa kwa mashabiki maana maamuzi mara nyingi yanayotolewa huwa sio sahihi.
Elimu ya kuhesabu points au kuangalia namna mshindi anavyopatikana ni vigezo gani au sheria zipi hutumika lazima mashabiki wawekwe wazi juu ya hilo.