Kenya 2022 Kwa yanayoendelea Kenya, Nyerere apongezwe kuondoa ukabila

Kenya 2022 General Election
Sky...
Tanganyika hapajapatapo kuwa na tatizo la ukabila tofauti na nchi nyingine za Afrika ya Mashariki.

Tatizo la Tanganyika ni udini na ukisoma historia utakuta tatizo hili lilizuka kwa nguvu baada ya uhuru mwaka wa 1961.
 
Nyerere alikuwa fundi sana kuondoa ukabila, chadema watasema tuna mengi ya kujifunza kutoka Kenya lakini hawawezi kuongea kuhusu ukabila unaowatenganisha wakenya

Sasa kama Wakenya wana ukabila na wana mifumo imara hivyo, je wangekuwa hawana ukabila ingekuwaje, si wangekuwa kama ulaya kabisa.
 
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Kenya (IEBC), Juliana Cherera na wenzake watatu wamesema hawayatambui matokeo ya uchaguzi mkuu yatakayotangazwa kutokana na hatua za mwisho kughubikwa na sintofahamu.
Hivi watu wa NEC wanaweza pinga uchaguzi unaofanyika tz

Ova
 
Hivi nyie mnaosema usipochagua ccm hatuleti maendeleo na ule ukabila mnaowalazimsha wakenya kuwa nao mnatofauti gani...???uvccm oneni aibu ....Nyie ilibidi mpige kimya tu kuhusu uchaguzi wa Kenya..
 
Tatizo sio katiba, Tatizo ni kwamba katiba haifatwi, hata wakileta katiba mpya unadhani itafatwa ??

Umenena vyema. Kuwa na katiba nzuri ni jambo moja. Lakini kufuata jinsi katiba nzuri inavyotaka, ni jambo lingine. Kama hatuwekezi kwenye utamaduni wa kufuata sheria, taratibu na kanuni (STK). Tukiendelea kuwa na jamii inayozoea kukanyaga sheria na kanuni, basi hata katiba ikiwa nzuri kiasi gani, haitakuwa na matunda mazuri.
 
Nyerere alikuwa fundi sana kuondoa ukabila, chadema watasema tuna mengi ya kujifunza kutoka Kenya lakini hawawezi kuongea kuhusu ukabila unaowatenganisha wakenya

..safari hii Wakenya hawakupiga kura kwa kuangalia kabila.

..Sikilizeni hotuba ya Raisi Mteule wa Kenya aliyoitoa leo baada ya kutangazwa mshindi.
 
Ujamaa umewafanya wabongo kuwa kama mazuzu

Ova
 
..safari hii Wakenya hawakupiga kura kwa kuangalia kabila.

..Sikilizeni hotuba ya Raisi Mteule wa Kenya aliyoitoa leo baada ya kutangazwa mshindi.
Bro uchaguzi wa safari hii ilikuwa ni kama kumkomoa mtu, usaliti uliofanywa na Kenyatta hakuna alioupenda
 
Hivi nyie mnaosema usipochagua ccm hatuleti maendeleo na ule ukabila mnaowalazimsha wakenya kuwa nao mnatofauti gani...???uvccm oneni aibu ....Nyie ilibidi mpige kimya tu kuhusu uchaguzi wa Kenya..
Ishu sio ukabila wa Kenya kuufananisha na mambo ya Uvccm ya Tz, ni kwamba upinzani/chadema bado sana kuongoza nchi bado hawajielewi
 
Bro uchaguzi wa safari hii ilikuwa ni kama kumkomoa mtu, usaliti uliofanywa na Kenyatta hakuna alioupenda

..ndivyo wapigakura wanavyotakiwa kuwa.

..kwamba ukiwazingua na wao wanakuzingua.

..Wakikuyu wamempigia kura Ruto na kuachana na ndugu yao ambaye amezingua.

..hapa kwetu kuna kiongozi ambaye alikuwa katili wa kutupwa lakini jamii yake ilimuunga mkono.

..Yule hata angekula nyama ya mtu mubashara kwenye luninga bado wafia kabila wangemuunga mkono.
 
Mwanzoni nilikuwa nampa nafasi Odinga ila nilipokuja kuona wanavopishana kwenye kura nikajua kabisa Odinga hatoboi
 
Wakati tz mnapambana na udini ni ujinga mkubwa zaidi
 
Mwanzoni nilikuwa nampa nafasi Odinga ila nilipokuja kuona wanavopishana kwenye kura nikajua kabisa Odinga hatoboi

..hata mimi haya matokeo yamenishangaza.

..nilitarajia Raila angeshinda kwasababu ya kuungwa mkono na Raisi Kenyatta.

..nasubiri wachambuzi wa siasa za Kenya watueleze ni nini haswa kimepelekea matokeo haya.

..kwa upande mwingine Raila hajashindwa vibaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…