Kenya 2022 Kwa yanayoendelea Kenya, Nyerere apongezwe kuondoa ukabila

Kenya 2022 General Election
Nakazia

We are because Nyerere J. K was a Prophet, Man of people and Father of everybody
 
Huu udini upo wapi mbona siuoni?
Ukikaidi...
Tuanze na maana ya udini.
Udini ni pale imani inatumika kufanya upendeleo kwa misingi ya imani.

Angalia mfano huo hapo chini:

''Lakini tuende kielimu. Ninayo ripoti ya mwaka huu. Waliofanya mtihani wa darasa la saba kuingia darasa la tisa, asilimia 71 Waislamu. Asilimia 29 ni wengine.

Walioshinda katika wale asilimia 71 ni asilimia 21.
Katika wale 29 walioshinda tena sema mwenyewe.

Katika asilimia 29 waliokwenda shuleni ni asilimia 79. Katika asilimia 71 waliokwenda darasa la tisa ni asilimia 21.

Sasa kuna moja, ama Waislamu wajinga ama akili yao haifanyi kazi, ama mtu ukiwa Muislamu wewe huna kitu, ama kuna kitu.

Sasa namwomba Waziri anayehusika, anaposema aseme ya kwamba kwa hali ilivyo Waislamu wameumbwa wajinga.

Au kwa hali ilivyo kuna sababu kadha, kadha. Mwalimu Nyerere alisema zamani ifanywe bidii ya kuwanyanyua waliokuwa chini.

Sasa bidii hii siyo ya kuwanyanyua waliokuwa chini. Bidii hii ni ya kuwakandamiza waliokuwa chini.''

(Hotuba ya Kitwana Selemani Kondo Bungeni Dodoma 1999).

Ikiwa wewe ni hao Wengine hakika haya hutoyaona kwa kuwa wanao watakuwa wanachaguliwa kuendelea na masomo kwa mtindo huo wa 21:79.

Huu ni mfano mmoja.

Mfano wa pili ni huo hapo chini baada ya Waislam kugundua hujma hii walifanya maandamano makubwa mwaka wa 2012 kupinga udini huu:

''Nipe ruhusa nikupe kisa kuhusu kesi ya maandamano ambayo vijana wengi
wa Kiislam walikamatwa kwa ''kuandamana.''

Maandamano hayo yalihusu kupinga dhulma za Baraza la Mitihani (NECTA) kwa Waislam.

Mmoja wa vijana waliokamatwa alipopata ruhusa ya kujitetea kabla
hukumu haijatolewa alimuuliza hakimu, ''Mheshimiwa Hakimu nini maana
ya kuandamana?''

Hakimu akamfahamisha.

Yule kijana akamwambia hakimu, ''Mheshimiwa hakimu mimi siku hiyo
nilikuwa peke yangu natembea karibu na Picha ya Bismini ndipo
nikakamatwa nikaja kujua baadae kuwa siku hiyo kila aliyevaa kanzu
alikuwa anakamatwa lakini mimi sikuwa katika maandamano.''

Huyu kijana na wenzake kama yeye ''wavaa kanzu'' wote walitiwa hatiani
na wamefungwa.

Huu ndiyo ukweli wa nchi yetu.
Muislam hana thamani na ndiyo leo tuka katika 20:80.''
 
Sio kweli saiv raisi , waziri mkuu na katibu mkuu kiongozi ni waislamu kwani haya hawayaoni na mwaka 2012 raisi alikuwa kikwete muislamu je naye alishiriki kuwakandamiza waislamu wenzake.
 
Nyerere kwa nafasi aliyokuwa nayo angeweza kabisa kuwateua watu wa kabila lake vyeo vikubwa, kupafanya alikotoka kuwe na maendeleo sana, n.k. lakini alijua kabisa angeafanya hivi hii ingezaa mbegu ya ukabila
Hapa ndo aliharibu. Angewateua tu wale shavu. Kwani nini bhana
 
Tanzania ni Taifa kubwa sana huwezi kulifananisha na Kenya. Japo kwenye ukabila na udini ni kweli Nyerere alituweka sawa.

Tukiacha UKABILA na UDINI, Nyerere alikosea sana kutuachia KATIBA mbovu namna hii na tume mbaya kiasi kile.
Katiba inarekebishika,Ila ukabila na Udini haurekebishiki hata kidogo, Kenya wamerekebisha Katiba lla bado ukabila unawatesa. Sisi tukirekebisha katiba, Mambo yote ni mazuri
 
Ni mwaka gani nchi hii ilikuwa na ukabila na Nyerere akauondoa mwaka gani?

Unawezaje kuondoa kitu ambacho hakijawahi kuwepo?
Tumpongeze mkoloni mjerumani hajatugawa kwenye makabila ,tofauti na mwingereza ambaye kwa makusudi aliwagawa wakenya kwenye makabila kwa madhumuni ya kuwatawala-divide and rule.
 
mfumo wa elimu pia ubadirishwe maana naona anakomaa kujenga madarasa mazuri tu na elimu bado mbov
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…