Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 11,557
- 33,535
Wakuu, huku tukiwa tunaendelea na shamra shamra za Uchaguzi mkuu. Kuna ukurasa unaojiita Mawaziri & Manaibu Tz. Dhumuni ya ukurasa huo ni kuonesha taarifa na habari mbali mbali za manaibu waziri wote Tanzania. Ukurasa huu umejiunga na mtandao wa Twitter mwaka 2018 na umekuwa ukituhabarisha taarifa mbali mbali muhimu kwa mustakabali wa nchi yetu.
Katika hali ya kushangaza ukurasa huo umekuwa katika majibizano kutetea serikali ya awamu ya tano dhidi ya moja wapo ya watumiaji wa mtandao huo. Majibizano hayo yanaonekana kufanywa na mtu mwenye gadhabu ambaye anaonekana wazi kabisa kuandika maudhui ambayo ni mtizamo wake binafsi na si wa serikali/mawaziri na makatibu wake.
Kuna umuhimu wa kuwapatia hawa waratibu wa akaunti hizi za zinazowakilisha serikali kwa jamii, wanaweza kuwa na nia njema ya kuitetea serikali lakini si kwa kujibizana mtandaoni. Serikali ni taasisi kubwa na inaweza kusikia mengi yanayosemwa lakini si kujibizana na kila jambo papo kwa hapo.