Kwa Zitto Kunang'ara na Daku Lake la Ramadhani Linang'ara

Kwa Zitto Kunang'ara na Daku Lake la Ramadhani Linang'ara

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KWA ZITTO KUNANG'ARA NA DAKU LA RAMADHANI LINANG'ARA

Zitto hajaacha kunishangaza kila siku.
Nilikuwa na hamu ya kuingia ndani ya Restaurant niangalie na kupiga picha.

Lakini kitu kimoja kilinifanya nishindwe.
Ndani ni sehemu ya faragha na nikahofia nisiingie ndani nikaingilia faragha za wateja wakiwa wanakula.

Siku zote nikawa naishia kuchungulia kwenye vioo na kwa hakika nilivutiwa na nilichokitia machoni.
Ndani kwa uhalisia wake kukoje?

Hili sikupata kujua hadi jana usiku inakimbilia saa tano.

Tarwehe imemalizika na watu wanakuja kwa Zitto ama kubeba daku au kula hapo hapo kwa wale wenye kula daku mapema.

Mie napita njia na hamsini zangu.
Ghafla nashikwa mkono naambiwa rafiki yangu ndugu Haruna Mbeyu yuko hapo kwa Zitto.

Ghafla tena na nyingine.
Mbeyu yuko mbele yangu na ''team'' ya vijana wenzake.

Tumesimama mbele ya mlango wa kuingilia Restaurant na Mbeyu keshaanza vurugu zake kama ilivyo kawaida yake.

Baada ya kusalimiana.
''Shemeji ingia tule.''

Hii kwa nini ananiita ''shemeji'' iko siku maalum nitaihadithia.
Kisa kina zaidi ya miaka 30 sasa.

Natoa udhuru.
Basi kaa tunywe juice.

Natoa udhuru.
Mbeyu anamtupia Zitto maneno, ''Huyu shemeji yangu.''

Ikanijia kuwa siwezi kumpita Mbeyu lazima nikaenae kitako ndani ya Restaurant tuzungumze mawili matatu ingawa muda ulikuwa umekwenda.

Mbeyu karejea tena habari ya chakula.
Nimekubali tumekaa kitako.

Nimeepiga ''order.''
Mbeyu kaongeza ''order'' nyingine.

Hii ''takeaway'' nipeleke nyumbani.
Alhamdulilah.

Sikujuta kukaa kitako na rafiki yangu.
Ikawa nimepata nafasi ya kukutazama ndani kukoje kwa mara yangu ya kwanza.

Mashaallah.
Panavutia.

Jichao langu limepiga kwenye ''mural'' ukutani ''pattern'' staili ya Picasso.
Nikitaka kumweleza Pablo Picasso na uchoraji wake tutakesha hapa.

Huyu ni bingwa wa ''abstract.''
Unaangaia picha huoni kitu.

Inataka uisukume akili yako wala si macho yako kuona picha katika picha ya Picasso.
Huyu Zitto ana mambo.

Anatuwekea Picasso Magomeni Mapipa...
Na kwa nini tusiwekewe kwani sisi si binadamu?

Sasa nimesimama.
Napiga picha.

Kuna picha nyingine.
Hii imenimaliza.

Picha ya Morris.
Narudi kukaa kitini kwangu.

Mbeyu ananijulisha kwa mwanangu mtoto wa ndugu yangu anajitambulisha.

Namwambia baba zako wote nawajua toka vijana mimi mtoto nasoma shule ya msingi wao vijana na wote walikuwa wacheza mpira wa sifa.

Huyu ni mjukuu.
Huyu anahitaji siku maalum kumhadithia.

Yeye na nduguye wameweka rekodi ya mpira wa vijana Uingereza.
Wamebeba vikombe.

Mpira uko ndani ya ukoo huu wa marehemu Akida Seif wa Tanga.

Namsikitikia huyu mwanangu kuwa hakupata kumuona baba yake mkubwa marehemu Hemed Seif alivyokuwa akicheza mpira.

Hemed Seif alifunga goli Tanzania ilipocheza na West Bromwich Albion ya Uingereza Uwanja wa Taifa katika miaka ya 1970.

Picha ya Hemed Seif anawatoka Waingereza anazinyanyua nyavu ilitokea katika gazeti la Tanganyika Standard.

A night to remember.
Never a dull moment with Haruna Mbeyu.

''Atmosphere'' ya Kwa Zitto inaongeza ladha ya kuku wake.
Allah amzidishie.

1741964832853.jpeg

1741964877930.jpeg

1741964932431.jpeg

1741964967625.jpeg
 
Back
Top Bottom