Kwahali hii TFF ijitazame sana la sivyo ligi kuu ya Tanzania haina hadhi ya kuitwa ligi bali ni kichekesho tu na kuibua malalamiko yasiyo na tija.

Kwahali hii TFF ijitazame sana la sivyo ligi kuu ya Tanzania haina hadhi ya kuitwa ligi bali ni kichekesho tu na kuibua malalamiko yasiyo na tija.

Malalamiko yenu yanazidi kadri ligi inavyozidi kuwa ngumu.
Bado vile viporo vya Yanga wakati wa Malinzi tunavikumbukwa, hasa ule msemo wa viporo vinaliwa kwa ndimu. Sipendi ukosefu wa utaratibu lakini nafahamu pia kuwa kuimba kupokezana
 
Malalamiko yenu yanazidi kadri ligi inavyozidi kuwa ngumu.
Bado vile viporo vya Yanga wakati wa Malinzi tunavikumbukwa, hasa ule msemo wa viporo vinaliwa kwa ndimu. Sipendi ukosefu wa utaratibu lakini nafahamu pia kuwa kuimba kupokezana
Yanga walikuwa na viporo vinne simba wakaenda TIFUATIFUA kulia. Sasa leo nyie viko 11 sawa na idadi ya wachezaji wenu. Hivi hiyo ni ligi gani duniani uliona huo upuuzi? Kwanini ligi isiendeshwe kwa kanuni? Sitaki kujua mm ni timu gani ila nataka ligi iendeshwe kwa kanuni.
 
Yanga waliomba wasicheze game zao away kwasababu walikua hawana pesa, mfano yanga ilibidi aanze na mtibwa morogoro yanga wakaomba ipigwe Dar, hivyo hivyo kwa mwadui na Coastal Union sasa ratiba zinawabana mbeleni mnaanza kulalamika.

Simba tumecheza na Js saoura jumamosi na jumapili tukacheza fainali tukapoteza na hatujalalamika. Hakuna masuala ya bodi hapa vyura hamjui mpira shame on you!!!
Mm nadhan hapa tusizngumzie usimba n uyanga,TFF wanamatatz sana,ligi mbovu n utawala mbovu....basi wanashindwa hata kukopi kwawenzetu kenya au uganda? Kabla ratiba kupangwa z ligi zote africa kwnz CAF wanatoa ratba yao,so kwnn wasiiangalie ratb y CAF ilvyo ndo wakapanga nawao ratba yao..
Shame on tifuatifua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasalaam!
Kwa wapenda michezo wote wa Tanzania. Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) ndilo limepewa dhamana ya kusimamia mpira wa miguu Tanzania kwa usawa na haki. Lakini kwa hali halisi na nikichukulia mfano hii ligi yetu bado TFF na wadau wa mpira (bodi ya ligi) wana kazi kubwa sana.

Ligi yetu inaonekana kutokuwa na maana hasa pale ushindani unapoonekana dhahiri kuzibeba baadhi ya timu na kuonea timu nyingine. Leo nimeamua kufuatilia mwenendo wa ligi nikashangaa sana kuona timu moja ina viboro 11. Tangu nizaliwe sijawahi kuona ligi ya namna hiyo.
Kwa mantiki hii sioni haja ya kuiita ligi maana kuna timu zinachoka wakati nyingine zinarelax tu. Ajabu nyingine ni kuona kuna timu moja imepangiwa mechi mfululizo 11 katika uwanja mmoja jambo ambalo linaondoa hadhi ya ligi. Kwa mantiki hii kuna haja gani ya kuwa na bodi ya ligi au shirikisho la mpira wa miguu kama.mambo yanaachwa yaende hivi?
Inakuwaje timu moja inasafiri mikoa karibia sita ndani ya wiki moja kucheza mechi tofauti ukichukulia hali halisi ya barabara zetu na ligi kukosa mdhamini?
Inakuwaje viongizi wa mpira wa miguu hawaoni haja ya kutengeneza uwiano sawa wa ushindani kwenye ligi ilihali wanajua kuwa ni kosa kisheria kwani inaleta malalamiko na kukatisha tamaa baadhi ya timu?
Nawaomba TFF waache siasa waangalie mpira wa Tanzania.
Al ahly ya Misri ilicheza na Simba jumamosi lakini jana imecheza mechi ya ligi. Ni kitu gani kinazuia Simba kucheza game zake? Na kwanini iwe mwaka huu tu wakati simba inashiriki kimataifa?
Je kama timu zikilalamikia yatakayotokea kwenye mechi za viporo ikifikia kuleta tuhuma za rushwa TFF watakwepaje huo mtego?
Naomba sana wadau wa mpira wa miguu waliangalie hili jambo kwa jicho la tatu la sivyo mpira wetu utakuwa wa hovyo hovyo mpaka mwisho.
Sioni haja ya kuwa na chama cha mpira wa miguu wala bodi ya ligi bali kilichopo ni ubabaishaji na uonevu kwa baadhi ya timu.
Shame on you TFF
Karia mwenyewe ni muimba mipasho tuu siku hizi anatafuta umaarufu kupitia Lissu
 
Simtetei yeyote kati ya Simba na Yanga, lakini kama kuna mtu alitetea Yanga kucheza mechi 10 uwanja mmoja akapimwe akili, na kama kuna mtu anatetea Simba kuwa na viporo mechi 11 akili yake ina walakini.
TFF hii haina tofauti na FAT ya akina Mussa ambayo baada ya Simba na Yanga kila moja kutaka mpira wenye rangi ya jezi ndio uchezwe waliamua kununua mipira miwili yenye rangi za kila timu na kuamuru kila mmoja utumike kipindi kimoja. Eti kura ikapigwa uanze mpira wa timu gani? Huu upuuzi ulinifanya niache kushabikia mpira wa kitanzania tangu siku hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom