Kwaheri Hans, Yanga tuache na vichaa wetu

Kwaheri Hans, Yanga tuache na vichaa wetu

Ni kocha mzuri. Ameleta transformation kubwa kwa timu ya Yanga ambayo haikuwa na utamaduni wa kuweka mpora chini.
Ameifikisha timu kwenye kiwango cha kushindana Afrika, tena akitumia wachezaji wengi wenye uwezo wa kawaida kulinganisha na washindani wao.

Nadhani alishahili heshima hata kama muda wake wa kuondoka umefika.
 
Kwaheri Hans hii ndio Tanzania, Kichwa cha mwendawazimu, wamekuletea kocha bila kuvunja mkataba na wewe, ni dharau kubwa, ukienda kwenu ulaya kawaambie kwanini mpira wetu haukui, kocha aliyeaminiwa na taifa kama kocha mkuu leo amekubali kuwa kocha msaidizi wa Yanga, Hans ukienda Ulaya kawaambie mpira tunaupenda kwa sababu tunaangalia sana wazungu lakini si kipaji chetu na ndio maana tulifungwa magoli 7 na waarabu, hawakutubahatisha bali ndio uwezo wetu, ukienda Ulaya kawaambie tunajua zaidi siasa na fitna za mpira kuliko kuucheza mpira wenyewe. Nitafurahi sana ukienda Azam ili uwaprove wrong management ya Yanga.

Kinachouma zaidi si wewe kuondoka bali njia iliyotumika kukuondoa. Wamekudharau sana kwa heshima uliyowajengea. Walichokufanyia Hans ni sawa na kuoa mke halafu amekuchoka na kuanza kukuingizia wanaume ndani halafu anakuambia ukalale sebuleni. Historia itawahukumu. Kabla hujaondoka subiri mechi tano za Yanga, kama mzambia akiharibu ataondoka yeye na Manji wake just wait n see.

Kila la Kheri Hans usisahau ule utafiti wa wizara ya afya wa kila watanzania 4 mmoja kichaa, Yanga tunafika watu milioni 10 wanachama na mashabiki sasa utafanya hesabu mwenyewe
View attachment 423860
Naona unaongozwa na mihemko na uvivu wa kufikiria
 
Yani Tanzania bwana nchi ya kis£ng£ Sana simba ikifanya vizuri yanga Ina migogoro na yanga ikifanya vizuri simba migogoro huu ni ujinga wa hali ya juu kwa team hizi mbili
 
nacho jua na nilicho kisoma nikuwa Hans atakuwa mkurugenzi wa ufundi
 
Yanga hapa mmepotea mnamuacha kocha kwa sababu ya Ngassa?
 
Mimi ni shabiki wa simba ila huyu kocha alikuwa mzuri sana kama wana sababu nyingine za kumtoa ikiwemo ushirikina sawa ila kama ni maamuzi ya kijinga basi watakula msoto mwaka huu.
 
Ukweli nimeumia sana kwa hili kocha ambaye alikuwa mleta changamoto za mpira daaah kwanza anaujua mpira wa EA daaah ngoja waone sasa lazima wafukuzane
 
Chaneta FC Kupitwa Kwa Points Chache tu Na Simba Wamefukuza Kocha! Je Mnyama Akapotwaa Ubingwa Mwisho Wa Msimu si Mutamnyonga Kabisa Huyo Kocha Mpya... 😀😀😀😀😀
 
Huyu asha ondoka , cha kuwaza anaye kuja ni bora zaid yake !!? Hilo ndo jambo la msingi
 
Speed kali sana isiyozuilika ya simba inawafanya hadi mnafukuza makocha hahaahaaha kwa staili hii tz.kuendelea katika mpira kimataifan ni ndoto ..mnataka.kua wa kimataifa huku mnafukuza makocha
 
Inaonekana mechi alizo shinda ni zile uongozi wa yanga ulizo honga marefa na wachezaji wa timu pinzani na wasipo honga wanafungwa.
Sasa kwa style hii huyo kocha wa nini.

Na wote ni mashahidi wa jinsi uongozi wa yanga unavyo honga.
 
Back
Top Bottom