Je, tunamzungumzia Trump huyo huyo au mwingine?😁😁
Trump 2020 hadi 2024 , Haipingiki hata ukichukia
-1973 alishitakiwa na kukutwa na hatia ya kufanya ubaguzi dhidi ya watu weusi kwenye real estate zake yeye na baba yake. MBAGUZI (jaribu ku-google Donald Trump Housing Discrimination Case)
-2005 alianzisha Trump University ambayo haikusajiliwa lakini ilishinikiza wanafunzi kuchukua mikopo mikubwa. Chuo hakikuwa na walimu wa kueleweka. 2010 Idara ya Elimu ilimwandikia barua kumjulisha kuwa amevunja sheria, na 2015 kesi ilifikishwa mahakamani dhidi yake. -TAPELI (jaribu ku-google Trump University)
-1989 Trump alijipatia kiki kwa kujitoa kuwaangamiza vijana weusi wanne na mlatino mmoja, wote wakiwa chini ya miaka 17. Trump alidai hukumu ya kifo dhidi ya vijana hao ambao baadae ilidhihirika kisayansi kabisa hawakuhusika na unyama aliofanyiwa mdada mmoja Central Park, New York. Hata baada ya ushahidi, Trump alikataa kabisa kukubali - MPUMBAVU (hadi sasa unaweza kuona kabisa, hata akiambiwa na wataalamu juu ya jambo, hataki kulijua au kufikiri. Mjinga atataka kujua, akijua basi yamekwisha. Si Trump; cheki majanga ya corona)
-Upumbavu wake umekuwa hatari kubwa. Kwa mfano pale alipopendekeza disinfectant ichomwe mwilini. Kuna wafuasi wanaomfuata kimaamuma wengine walikufa au waliishia ER. (unaweza ku-google disinfectant injection death).
-Trump mara kadha ameonekana kutoifahamu historia ya nchi yake. Juzi amedai Flu ya 1918 (yeye akidai ni ya 1917) ilisababisa vita vikuu vya pili vikome kwa sababu maaskari wote walikuwa wagonjwa. Tunajua vita hivyo vilianza 1939 kwisha 1945. Pia aliwahi kutamka kwamba katika vita kupambana na dola ya Uingereza (karne ya 18) wapiganaji walilinda viwanja vya ndege. Ilhali ndege za kwanza ziliundwa mwanzoni mwa karne ya 20. - JUHA
-Baada ya Obama kuchaguliwa kuwa raisi, alikuwa msitari wa mbele kudai kwamba Obama hakuzaliwa Marekani. Alidai hadharani cheti cha kuzaliwa Obama. Hakuna raisi hata mmoja amewahi kudaiwa hadharani. Kufikia 2011, Obama alilazimika kutoa cheti chake hadharani. Trump hakukubali, hapo akaanza kwanza Obama alipataje nafasi ya kusoma Columbia na Harvard, na kwamba atoe transcript kuonesha uhalali wake kusoma huko. Tena, hakuna kiongozi amewahi kudaiwa hayo. Yote hayo ni kuashiria kwa supremacists wenzake kwamba huyo ni mtu mweusi na hastahili - MWONGO na MNAFIKI.
-Unafiki wake hasa kwa mambo ya dini. Nitasimulia wakati mwingine.
-Kila kitu kinatafsiriwa kwa mujibu wa maslahi ya Trump. Ndiyo maana corona inaitesa Marekani. Ilipoanza, alidai kuwa huo ni uzushi uliokusudiwa kumwangusha. - HANA STADI ZA UONGOZI kwa sababu ya UBINAFSi
-Bankruptcy je, utapeli kwa watu mbalimbali je? remember grab they by the p***y?
Jiulize pia kwa nini anapendwa sana na wabaguzi kama KKK na makundi kama hayo. Na kwa nini unayemsema mbaguzi Biden hapendwi na hao white supremacists.
Ushauri: Tafuta vyanzo mbalimbali vya habari. Social media ni echo chambers. Huwezi kupata taarifa anuai na zenye kuchambuka ukweli wake. Zina confirmation bias. Usikubali habari za vijiweni tu. Tafuta vyanzo vya kuaminika. Kanuni moja ya kiuandishi, jaribu kuthibitisha habari kutoka sources tofauti.