Kwaheri wana Dar es salaam, Tunashukuru kwa matusi yenu

MATHIAS KABYEMERA

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2013
Posts
1,793
Reaction score
572
Wiku hii wakazi wa Dar es salaam mliokuwa mmekuja kula sikukuu mikoani mnaanza kurejea makwenu. Tunashukuru kwa matusi yenu kuwa sisi ni washamba, hatujui kuendesha magari wakati mmekodi magari yetu n.k

Inashangaza sana. Hawa jamaa ni wazaliwa wa huku, unakuta sisi tuna maisha bora kuliko wao kwani tumejenga hatupangi, tuna usafiri wetu hatuazimi wa mtu, hatuna madeni kama wao, tunaishi wa umoja, upendo na maelewano. Wao wanakuja kwenye sikukuu wanakuomba uwaazime gari, wanakuomba uwapeleke kwenye “kiwanja” kinachowika ili wafurahie. Wakifika hapo wanataka kila mtu atambue kuwa katoka DSM. Wanatukana wahudumu, wanachambua mavazi ya wateja n.k.

Ndio maana nasema KWAHERINI TUACHE JINSI TULIVYO!
 
Mkuu bajeti yako ya miezi mitatu ni kiroba cha mahindi na 20,000 Tsh.

Usipokua na maisha mazuri umeyataka mwenyewe.
 
watu wa mikoani kila kitu wanalalamika
 
Hahahaha Watakuwa Wamekusikia Mimi Kuna Yule Jamaa Yangu Yumo Humu Anajiita Bitoz Alikula Mpaka Nauli Anataka Nimpe Ili Hali Huwa Ananichamba Mimi Mchunga Mifugo Eti Nimpe Au Ndiyo Alowee Mwanza Mazima?
 
Natumaini mmepiga piga picha za ukumbusho.
Daraja la manzese, daraja la ubungo, jengo la tanesco na picha za baharini.
Haya nendeni, mtuachie mji wetu!!
 
Vinuka jasho tuachieni mji wetu mjitahidi mnunue hata Deo Spray unapokea mgeni nyumba nzima inanuka kama zizi la beberu heri mrudi maporini kwenu mkalime sisi tutanunua unga hatununui mahindi.
 
Vinuka jasho tuachieni mji wetu mjitahidi mnunue hata Deo Spray unapokea mgeni nyumba nzima inanuka kama zizi la beberu heri mrudi maporini kwenu mkalime sisi tutanunua unga hatununui mahindi.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] hiki kichambo.
 
Kuna mtu kaniuzia simu ya 180000/= kwa 30000/= huku kilema moshi anataka imsaidie adandie maloli pale njiapanda himo arudi dar,japo alipofika tar.24/12/2017 sie wote tunaoishi Kijijini tulionekana washamba tuliovunja rekodi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…