Zanzibar 2020 Kwaheri ya kuonana CCM

Zanzibar 2020 Kwaheri ya kuonana CCM

Salaam kutoka Zenji ,kuna uhakika kutoka kila pembe kuwa sasa ni rasmi CCM imeshazikwa Zanzibar,hilo halina mjadala ,jukwaa la CCM Zanzibar CCM huchawanyika na kumuwacha/chia baba na mwana kwenye jukwaa.
Huyu baba ameenda kufanya nini mbona anamharibia mwanawe ? Husein unahisi ana ukakasi fulani ,huwezi kurapu ukaeleweka kama mzee wako yupo pembeni.

Ukweli ni kuwa CCM haipo imeshafutika kwa wananchi ambao ndio wapiga kura,kila lifanywalo na kupangwa na kina Bashiru kutoka Tanganyika huwekwa uwanjani,mipango na mbinu zote zinajulikana na wananchi sasa kama wananchi au tuseme WaZanzibari walio wengi wanajipanga kupambana na hila hizo ovu,

CCM ijue Zanzibar watu wao wanauelewa wa uraia wao na hawababaiki na mambo ya siasa wanaangalia zaidi muelekeo wa Nchi yao na hatari inayoikabili ,kusema kweli CCM wamevuruga kumuweka Husein Mwinyi,wangeweka nokoa yeyote yule Mzanzibari kuliko kumuweka mtu ambae hata mitaa ya Zanizibar haielewi,na kusema kweli wamempa wakati mgumu sana Husein Mwinyi ,sasa hajui achague nini kati ya dini na dunia.

Mipango ya Bashiru au tuseme CCM yote ipo njenje na inaeleweka tena inaeleweka hatua kwa hatua,kuna ulazima gani kulazimisha ushindi ? Kwamba ni lazima CCM ishinde,wakati haikushinda chaguzi zilizopita ambapo kulikuwa na wagombea waZanzibar atakuja kushinda huyu ambae CCM wenyewe wametifuana ndani wenyewe kwa wenyewe na hawajakaa sawa hadi leo.

CCM acheni mbinu chafu mtaumbuka na mpira utakuja kuwaangukia watumika.
Uchaguzi wa mwaka huu huko Zanzibar tuombe tu mungu yasitokee makubwa 🙏🙏🙏
 
Hilo ndio tatizo la CCM mnavamia na kumvaa mtu,sasa wewe kwa akili yako Maalim Seif unaweza kumkisia ana umri gani labda tukitumia hesabu za Mtume Muhammad Salallahu alaihi wasalamu wastani wa umati wake ni miaka 70 hapo unacheza na plus au minus tu.

Kwa hiyo ili Maalim asitawale au asiwe kiongozi inabidi CCM mpo tayari kuuwa ,sasa kwa hesabu zenu hizo mjue hampambani tena na Maalim Seif mpo na mnapambana na umma wa Wa WaZanzibari Maalim yupo katika extra time tu japo ninaweza nikafariki mimi au wewe maana sio ajabu kuanguka korokochi ikabakia nazi juu ya mnazi..
Wao akili zao wanawaza wataishi milele hata kwa EL waliyatamka hayo matokeo yake wengi wa wapendwa wao wamemtangulia!!!
 
Back
Top Bottom