Kwahiyo kama Taifa tumekubali kuwa bodaboda ni kazi rasmi?

Kwahiyo kama Taifa tumekubali kuwa bodaboda ni kazi rasmi?

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari!

Kila kona kijiwe cha bodaboda. Kila kwenye kauwazi kijiwe cha bodaboda. Haya ndiyo maendeleo? Kwamba watu hawana mawazo mbadala zaidi ya kuwa bodaboda? Kwamba serikali imehalalisha bodaboda kuwa ajira rasmi?

Watozwe kodi basi kama ni ajira rasmi. Wazee kwa vijana sasa wamekuwa bodaboda. Idadi ya vijana wenye mguu mmoja mitaani inaongezeka taratibu, vifo vya bodaboda navyo haviko nyuma.

Nashauri serikali kuwatoza kodi bodaboda na kuwafidia pindi wakipata ajali na kuwa na ulemavu wa kudumu. Wakifa familia zao zilipwe.
 
Uhalisia ni uhaba wa ajira na ugumu wa maisha mtaani bodaboda unapata pesa ya chap familia inapata mkate wa kila siku na maisha yanaendelea.

Halafu sio vijiwe vya boda tu mbona kuna vipub kila mtaa na mamlaka zipo kimya tu, yaani hivisasa kila mtaa unakuta kuna pub kama sio mbili ni tatu yaani ni full makelele ya walevi na mziki.

Suala la ajali, kuvunjika na kuwa mlemavu inaweza kukupata hata kama sio bodaboda, heshimu kazi za watu🤣
 
Bodaboda inalipa zaidi ya uwalimu by Mpwayungu Village
Tatizo ni kwenye ku-add value kwenye uchumi, bodaboda wanaolandalanda na kukesha kwenye vijiwe wangetumika kwenye shughuli za uzalishaji kama kilimo, ufundi, uvuvi, viwanda, useremala, ujenzi, uchimbaji madini, kuendesha bandari nk. nchi ingekuwa mbali sana kiuchumi.
 
Na asilimia kubwa ya hao bodaboda unakuta sio za kwao ni mikataba kwa hapa Dar ni miezi 14 kwa hesabu ya 10K daily.
Just imagine;
10,000/= ya boss daily
7,000/= ya petrol daily
5,000/= msosi kwa bachela daily
10,000/= masosi kwa aliyeoa daily
5,000/= mchezo wa upatu daily
*5,000/= smart, sigara au kuhonga daily
Kwa bachela Total 32,000/= daily
Kwa aliyeoa Total 37,000/= daily
Na wana wanafamilia, michepuko na wanatoboa mikataba na maisha yanasonga.
Hapo kwenye bold kuna baadhi sio walevi, malaya wala wavuta sigara.

Leo hii mnasema boda ni laana aisee mkajitafakari, wana mtaani wanapush hili life kibishi sana.
 
Tatizo ni kwenye ku-add value kwenye uchumi, bodaboda wanaolandalanda na kukesha kwenye vijiwe wangetumika kwenye shughuli za uzalishaji kama kilimo, ufundi, uvuvi, viwanda, useremala, ujenzi, uchimbaji madini, kuendesha bandari nk. nchi ingekuwa mbali sana kiuchumi.
Hivi unaelewa ulichokiandika mkuu
 
Bodaboda inalipa zaidi ya uwalimu by Mpwayungu Village
Ni kweli maana Bodaboda wana bima serikalini
Bodaboda Wanakopesheka kirahisi
Boda boda Wana uhakika na kipato chao
Bodaboda Wakistaafu huwa wanapewa pensheni
Bodaboda wanapata muda mwingi wa kufanya shughuli zingine za uchumi na familia.
 
Baadhi ya watu,hawawazi hilo,wao wanaangalia eti amepata pesa,pasipo kuangalia athari za hiyo njia ya upatikanaji pesa.Ni rahisi kupata taarifa za bodaboda hata 20 kwa leo tu,waliovunjwa miguu,kuliko kupata taarifa za mwalimu aliyejeruhiwa akiwa anatimiza majukumu yake.Hii kazi ya bodaboda,ifanyike kukiwa hakuna namna,na siyo viongozi wakae huko,washauriwe kua hakuna haja ya kutilia mkazo,utoaji wa ajira rasmi,kisa kuna shughuli ya bodaboda.Watu wawaze kua bodaboda,ina madhara makubwa,kwenye mwili wa muendeshaji,na itambulike kua hana hata BIMA ya afya,hana pension,hakopesheki kirahisi,hana muda wa kukaa na familia n.k.
 
Back
Top Bottom