Kwahiyo Ndugai na Chamuriho ndio mliutaka Urais miaka 2 iliyopita?

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
9,846
Reaction score
20,319
Miaka miwili iliyopita siku kama hizi hawa mabwana wawili Chamuriho na Ndugai waliutaka Urais kwa udi na Uvumba.

Ndugai alikuwa ashajiandaa kabisa kuwa Rais na kukaa Ikulu Chamuriho naye aliahidiwa Uwaziri Mkuu, lakini Mungu siyo Bashiru wala John Pombe waliotaka hayakuwa leo hii Rais ni Samia Suluhu Hassan watake na wasitake.

Zile zama za kutekwa, kupotea na kupigwa risasi hazipo tena, nchi imetulia kila mtu anafanya Siasa za kistaarabu atakavyo.

Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa Legacy ya yule bwana imefutika na kupotea mazima! Sasahivi wananchi wanaujua ukweli kuhusu yule bwana.

Ndugai na Chamuriho mnastahili aibu na anguko mlilolipata, huyu Chamuriho naye ni wa kumuhoji hayo mabilioni aloyajaza kwenye akaunti za nje aseme alizitoa wapi!

Huyu na Hayati walikuwa chanda na pete, huyu nae walishirikiana na hayati kuzidisha mapesa ya miradi ili wapige kupitia makampuni yao uchwara.

Awamu ya 5 nchi ilinuka ufisadi wa Hayati Magufuli, pesa ziliwajaa kufuru hadi wakaenda kuzificha China, Canada, na Malaysia.

Hata mshipa wa aibu hakua nao, nyingine zilikutwa Chato zimejazwa kwenye mifuko na majaba, aibu kweli. Tena nyingi zilikua ni Dola za Kimarekani, huku akituambia tuwapuuze mabeberu na vibaraka wao huku yeye akijaza Dola za Kimarekani huko kwenye mifuko na majaba Chato halafu kuna watu wanaamini eti alikuwa Rais wa Wanyonge!

Wanyonge wa Hayati ni kina Bashiru, Makonda labda, uharibifu aliyotia kwenye taifa huyu mwendazake itachukua miaka mingi nchi kujiponya, hadi leo najiuliza ilikuaje akawa Rais?
 
Unamzungumzia marehemu asiye weza kukujibu chochote,amelala mazima wala hataamka tena.

Shughulika na waliopo kushughulika na hamna ni upotevu wa muda usio na msingi wowote mkuu, tafuta pesa mkuu legacy yako italindwa na chawa wako.

Narudia tafuta hela mengine ni mbwembwe tu.
 
Ana watetezi kibao ambao huwa wanamtetea mtu asiyekuwepo.
 
HATA KAMA KALALA LAZIMA ASEMWE TU KWANI YEYE NDIYE ALIYEYATENDA
 
Upumbavu mtupu hv hamnaga kazi za kufanya!!? Majobless ni mengi Tanzania.
jitu kama hili unakuta linakaa kwa shemeji. What's wrong for a man to hv ambition!!??
ww ndio wale wa kupewa.
 
Zile zama za kutekwa kupotea na kupigwa risasi hazipo tena, nchi imetulia kila mtu anafanya Siasa za kistaarabu atakavyo
===
Siasa za kistaarabu nukta Habari za namna hii mkato kama nilivyonukuu hapo juu mkato ndizo zinachafua hali ya hewa nukta Lifanyike jambo la haraka ili kama ni uzushi usambazwao kwa hila mkato wazushi washughulikiwe mara moja nukta
 
Mtu wa Mungu kama mimi niwe upande gani? Niseme nini?
 
Ila watanzania aisee mmmh sometimes tuwe na staha basi unaandika vitu kana kwamba ulikuwa ikulu.
 
Sawa nyie tukaneni tu, ila muwe mmeshaandaa sehemu za kukimbilia soon.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…