Kwai hyo Millard Ayo ameshindwa kulipia server ya blog?? Nyie kweli blog hazilipi

Nadhani hajailipia kwa sababu ile trending ya watu kuingia kwenye web/blogs kusoma habari imepitwa na wakati.
Watu wanakesha Twitter, insta na TikTok, sema wenye viroho vya korosho sasa
 
kimsingi blog sio kitu kinachotembelewa na wabongo wengi kwa sasa. wengi ni inster, wale wachache facebook na wengi ni youtube na tctoc.
 
Blog ni zilipendwa, sikuhizi wachapishaji wa habari na wasomaji wamehamia kwenye mitandao ya kijamii instagram, youtube, facebook, twitter.
 
Yuko smart sana. Kama kitu hakikulipi achana nacho. Mitandao ya kijani imeshika htamu hakuna namna utarudi kwenye uzamani.
 
Kuna mmoja Jana alisema Millard ayo anaingiza mpunga mrefu kweny media yake Ivo tuachane na kilimo tukawe kama Millard
Lile ni andazi mkuu! Halafu jitu linapinga kilimo na ufugaji huku lenyewe bado liko kwa shemeji yake! Linasahau hapa mjini kuna manguli wa ufugaji kuku wanapiga hela kama hawana akili nzuri,
 
mkiacha unafiki, nyie mara ya mwisho kuitembelea hiyo website ni lini?
Mimi nilikuwa naitumia kusoma vichwa vya habari vya magazeti, kwahiyo daily asubuhi nilikuwa naipitia, sasahivi siipati almost 2moths
 
Tatizo la webisite ya millard ni tatizo la kimtandao ambao limezikumba website kadhaa zilizokuwa zinahost kwenye kampuni husika . Site nyingine zilizokumbwa na changamoto hiyo ni mtanzania digital n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…