Kwako Beki Dickson Job japo Mimi ni mwana Simba SC, ila kuendelea Kucheza Kwako NBC Tanzania Premier League ni sawa na Kututukana Watanzania

Dickson Job ni bonge la beki. Lakini atapata shida sana kwenda kimataifa kutokana na urefu/kimo chake. Iwapo akiamua kujilipua na kuchezea mbavu ya kulia basi sina shaka na yeye kutoboa kimataifa. Kingine cha muhimu kwake ni lazima aongeze kuujenga mwili wake kwani kwenye mpira pamoja na matumizi ya akili sana amabayo Job anayo lakini kuna wakati matumizi ya nguvu yanahitajika sana.
 
Daaa Leo umeongea jambo la maana na lenye akili kubwa sana big up mkuu
 
Mwili gani unausemea job ni mwembamba kama kina inonga?
 
Bahati mbaya sana kwake moja ya vigezo vikubwa vya beki wa kati kwa wenzetu ni height,na dogo anakosa iko..
Wenzetu wana prefer zaid mabeki wa kati aina ya kennedy,mwamnyeto ambao wanaeza kuku offer vitu vingi ndani ya box,
Kennedy ni bonge la beki anazo sifa zote.
 
Itakuwa kuna mtu kakuandikia
 
Kennedy ni bonge la beki anazo sifa zote.
Sasa kama ana Sifa zote Leo hii si angekuwa PSG au FC Barcelona au Liverpool FC Ndugu? Siku nyingine usirudie kusema kuwa Mchezaji fulani ana Sifa zote wenye Akili watakudharau kwani hata hawa Magwiji wa Kizazi hiki akina Messi na Ronaldo japo ni Mahiri ili hawajakamilika kwa 100% na Kisayansi mpaka Kiumbaji wa Mungu hakuna Mwanadamu aliye 100% perfect.

Mimi ni Simba SC kama Wewe ila kwa kusema Beki Kennedy Wilson Juma kakamilika 100% nakataa kwani ana Matatizo makubwa Matatu ya Kimsingi 1. Kuruka mipira ya Juu, 2. Mzito katika Kugeuka na 3. Hana Kasi kitu ambacho Siku Simba SC ikikutana na Mafowadi Viberenge watamtesa mno na tutafungwa sana.
 
Matatizo yote matatu Haya kuonekana siku ile tulipocheza na Benin kwao.

Ni mrefu na ana mwili mkubwa hizo ni sifa za ziada zinazomuuza Ulaya kwa sasa. Job hana hivyo vitu na ni vigumu kwake kuuzika huko nje.

Mtazame Kennedy halafu watazame mabeki wa Senegal au Cameroon.
 
Bahati mbaya sana kwake moja ya vigezo vikubwa vya beki wa kati kwa wenzetu ni height,na dogo anakosa iko..
Wenzetu wana prefer zaid mabeki wa kati aina ya kennedy,mwamnyeto ambao wanaeza kuku offer vitu vingi ndani ya box,
Hapana ndugu ukiwa na kipaji unadundatu Kama kawa hata mjerumani lahm alkuwa na kimo Kama Cha job
 
Hapana ndugu ukiwa na kipaji unadundatu Kama kawa hata mjerumani lahm alkuwa na kimo Kama Cha job
Fanya reserch kabla kubishia mkuu,
Lahm anacheza namba ngapi,
Iko hivo wenzetu wana prefer mabeki wa kati wenye vimo wanafaida nyingi kuliko wafupi,
Namba nyingne utacheza ila sio kati,
Fanya reserch yako ndogo alafu urudi hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…