Kwako Eng. Hersi Said taarifa hii ikufikie kuhusu chawa wako

Kwako Eng. Hersi Said taarifa hii ikufikie kuhusu chawa wako

Mr_Plan

Senior Member
Joined
Oct 2, 2021
Posts
140
Reaction score
194
Popote ulipo nakupa pole Rais wetu kwa mapambano unayopitia katika kutetea chapa ya Yanga.

Kufeli kwetu katika mambo mbalimbali yaihusishayo klabu yetu tatizo kubwa ni hawa machawa wako wanaokuzunguka, mdomo mwingi, sifa kibao utendaji sifuri.

Hao wamekuwa wakiangalia matumbo yao tu na kufunika ukweli kwa uongo ili bora liende ilimradi mifuko yao imenona.

Kuwa nao makini hawajui fitna yoyote ya mpira zaidi ya propaganda tu.

Wanakufelisha Rais achana nao wekeza kwenye timu, wanashauri zitoke bahasha halafu wanakata asilimia zao juu kwa juu.

Langu ni hilo.
 
Mbona Rais wenu nae kuna vingi alifeli, kwanini leo ionekana ni sababu ya machawa?

Kaeni mjipange muone wapi mlipokwama ili msonge mbele, sio muda wa kutafuta mchawi.
 
Mbona Rais wenu nae kuna vingi alifeli, kwanini leo ionekana ni sababu ya machawa?!
Kaeni mjipange muone wapi mlipokwama ili msonge mbele, sio muda wa kutafuta mchawi.
Vingi anavofanya anashauriwa na hawa Chawa Wachumia Tumbo
 
Mambumbumbu wenzangu toka MAKOLOKOLO FC chonde chonde tusijisahau sana maana mwisho wa safari yetu hauko mbali sana [emoji28]
 
Back
Top Bottom