Kwako Hassan Mwakinyo

Mbegu Jr

Senior Member
Joined
Sep 23, 2020
Posts
152
Reaction score
178
Mwakinyo wewe ni mtu imara sana nimeielewa kazi yako kweli una uchu wa mafanikio nguvu unayo ya kutosha

Wanaotaka kila siku mapambano wa wewe wakuwekee mapesa ya kutosha ndio upambane.

Nimesikia umesema unataka kumshuka mtu ukipambana naye pale Us yes pale ndio penyewe unaijenga brand yako vizuri kwa mapambano unayotupatia sisi watazamaji i am your number 1 fan.

Wanaotaka wapigane na wewe kwa hapa ndani kuna wanatutafuta maneno tu hata kwenye mpira ligi za nje zinazoshiriki timu zetu ndio zina faida kubwa hizi za ndani c unaona mwenyew kuaibishana na kushushana thamani tu ndio kilichopo nenda Marekani pale kwa Biden ukamnyooshe mtu wakulipe angalau dola milioni kadhaa najua unamtamani Mayweather pambana tu ipo siku watalitangaza hilo pambano

Mengine yatakuwa ni ziada tu .
 
Hongera kwake MWAKINYO....

Ila kubwa ninajiuliza....mbona anapenda sana KUACHA USO na kumpa muda mpinzani wake AMSHAMBULIE?!!!

Yaani ni Kama zile style za Al marhum hayati Cassius Clay Muhammad Ali?!!!!

Je, haoni kama kucheza hivyo kutamhatarisha SIKU akipigana na BONDIA BORA zaidi ambaye ana NGUMI ZITO...mwenye flexibility ya kushoto na kulia...mwenye SPIDI na mkwepaji zaidi (Kama alivyokuwa Oscar De La Hoya na Manny Pacquiao).

Pia afanyie KAZI flexibility ya PANDE ZOTE kulia na kushoto...

Ninamuona kama hayuko VIZURI kutumia Upande wa NON ORTHODOX na kutegemea zaidi AMALIZE kwa ngumi za UPPER CUT ya kulia pale MPINZANI wake anapoingia kizembe....

Afanyie Sana mazoezi kuhusu hayo...kwani siku akipata BONDIA aliyefanya mazoezi sana,mwepesi na mwenye NGUMI NZITO,na aliyeusoma UPIGANAJI was kipenzi chetu MWAKINYO basi atampa CHALLENGE Sana....

All and all Mwenyezi MUNGU azidi kumsaidia BONDIA wetu kipenzi Hassan Mwakinyo aaamin aaaamin.

Tuko nyuma yako na tunapenda kuona MAFANIKIO YAKO ndugu yetu!!!

BRAAVOOOO

KUDOOOS....
 
Yes Mwakinyo namkubali. Asibweteke, afanye mazoez, training na practice za kutosha atafika mbali
 
Namshaur kaka yetu Tarimba ampeleke Mwakinyo uk akajifue huko
 
kutamani kupambana na mayweather ni kutafuta mauti,mwakinyo bado ana safari ya kusafiri,
 
Hyo bondia aliyepigana nae mmeangalia matokeo ya mapambano yake ya mwisho? Kapigana na kiumbe dhaifu
 
Ushauri mzuri..na kama anapambano US basi itakua bomba pia, atafute wenye mikanda mingine katika uzito wake aombe mapambano nao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…