Kwako Jordan Henderson

Its Pancho

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
15,966
Reaction score
26,404
Kiukweli nimekaa nikawaza sana kuhusu huyu mwanaume Jordan Henderson.

Najua kuna watu hawampendi, wanaona kiwango chake kidogo, kiko chini mno, hafai kuwa Liverpool.

Nimemchunguza toka alipopewa beji ya u captain. Nimegundua Henderson ni mchezaji muhimu mno kwenye mfumo wa Klopp, that's why huwa anampamga gem kubwa kubwa.

Ana spirit ya uongozi, ana moyo wa kujituma mpaka tone la mwisho pale anapokosea. Move, pressing yoyote!

Hiyo ndiyo maana ya uongozi. Kuwa mfano kwa wengine! Henderson anafanya, anacheza vile ikiwa ni maelekezo ya kocha Klopp ndiyo yanamtaka awe hivyo. Na siyo kwamba ndo alivyo.

Tena sasa hivi ame-improve vizuri mnoo tofauti na mwanzo. Angalia move zake, pressing, anavyo-secure line japo anacheza kiungo ya juu, na nafasi hatengenezi nyingi. Ila anafanya kile alichotumwa na kocha.

Siongelei kuhusu cross matata aliopiga mechi na City, bali alivyocheza siku ile. Kama uliangalia vizuri baada ya Henderson kutoka nje kule kwa TAA akawa anazidiwa na Sterling mpaka Gomez akaja kumtuliza.

Tumheshimu captain japo hana mambo matamu kama ya "Captain Fantastic" Steven Gerard.

Apewe heshima yake. Maamuzi ya kocha yaheshimiwe.

Pancho boy
 
Tatizo la kapteni wetu Hendo ni maji kupwa na maji kujaa,gemu na Man City alikuwa kwenye kiwango bora.
 
Kichwa cha habari umeandika Kwako Henderson!

Nilitegemea unaandika ujumbe kwenda kwake, kumbe unatuandikia sisi kuhusu yeye!
ulitaka niandike kwako flan, flani niwataje wangapi??

haya nimemuandikia Hendo mbona ume comment?

bando ni langu huna haki ya kunipangia niandike nini!
 
ulitaka niandike kwako flan, flani niwataje wangapi??

haya nimemuandikia Hendo mbona ume comment?

bando ni langu huna haki ya kunipangia niandike nini!

Bro wewe ni mshabiki wa Liverpool kama mimi, sijakosoa mtazamo wako (Ingawa ni mtazamo wa kijinga).

Nimekosoa uhusiano wa kichwa cha habari na habari yenyewe.

Kama hujaelewa point yangu, sina ninachoweza kukushauri zaidi ya "rudi kamalize shule".
 
naona tufanye umeshinda kuepusha mengine bro.

nakubali narudi shule sasa. na mtazamo wangu ni wakijinga.. πŸ™πŸ™πŸ™
🚢🚢🚢🚢
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…