Kwako Katibu na Mwenyekiti wa CCM Kisarawe

Kwako Katibu na Mwenyekiti wa CCM Kisarawe

KIBWENZI

New Member
Joined
May 20, 2020
Posts
4
Reaction score
2
Hongereni kwa majukumu,

Kumekuwa na mchezo mchafu wilayani juu ya mchakato wa uchaguzi ngazi ya udiwani.

Kuna makundi fulani yanayoundwa na madiwani wanomaliza muda wao yanaanda orodha ya wajumbe wa chama matawini kutoka mifukoni mwao na kuwaacha wajumbe halali waliochaguliwa wenye vigezo vya kuwachagua wagombea wa udiwani kwa tiketi ya CCM.

Wajumbe halali waliochaguliwa wanaondolewa na kuwekwa wajumbe pandikizi kwa lengo la kuhujumu utaratibu bora uliowekwa na chama.

Niwape angalizo tu kwa makundi hayo yenye hila kwamba orodha ya wajumbe wote halali wa matawi waliochaguliwa inafahamika.

Hujuma hiyo ovu imeshajulikana na wanaoratibu mbinu hiyo wanatakiwa kuacha mara moja.

Pia niwaombe viongozi wa chama wilaya na hata mkoa kulifuatilia hili mapema ili lisije kuharibu mchakato wa uchaguzi ndani ya chama.

"Kunogile ukae"
 
Back
Top Bottom