mlikutana wapi na x wako?
mahusiano yenu yalianzaje?
kipi kizuri unakikumbuka kutoka kwake?
naomba majibu plz Mr
Gily
Sent using
Jamii Forums mobile app
Nilikutana na ex nikiwa chuo mwaka wa kwanza, siku ya kwanza kumuona nilitamani sana kuzungumza nae. Mie usione navyojieleza hapa ukazani ni mashuuri kwenye kutongoza hapana, nilikuwa zege kweli kweli. Mbali na hivyo mie sio mtu wa kuhangaika na wanawake. Basi nikajisogeza akiwa na rafiki yake, ila nilikuja jua hawakuwa friends nao wamekutana tu, basi wakati tunapiga story hizi na zile yule rafiki akawa amenichangamkia sana. Yeye alikuwa form six na pale mwenge alikuwa amekuja tution kusoma, basi tuakajikuta na story za hapa na pale na ushahuri mwingi tu. Kilichonipa sifa ni kuwa form six nilipiga PCB so akawa anavutiwa sana na jinsi nilivyosoma hivyo na yeye alikuwa anasoma PCB, na alishangazwa kwa nini chuo nimekimbilia biashara, Bachelor degree in Accountancy
Niliomba number zake, na nikawa namtumia message, kila message ikiingia iliyotoka kwake basi moyo wangu ulikuwa unadunda, kwa shauku ya kutaka tu kujua anachkisema ni kitu gani. Mungu ni wa ajabu sana, kumbe wakati mimi nimemzimia kumbe na yeye alikuwa kama kanipenda vile. Tukajikuta tumekuwa kwa mahusiano. Mahusiano yanapokuwa machanga unakuwa na hamu sana ya kutaka kujua cha ziada kutoka kwa mwenzako na yalivutia sana, ilibidi arudi shule. Basi akawa anarudi likizo na mapenzi yanakuwa matamu zaidi, shule nilikuwa napigiwa simu na number za walimu anadanganya anampigia mama yake, nilikuwa najisikia ananipenda sana sana sana na likizo nilikuwa natamani sana kuwa nae, na nilifurahi sana.
Nakumbuka yeye ndiye mtu wa kwanza kabisa kuninunulia keki kwa birthday yangu. Hakuna ambaye alishawahi kuninunulia kabla ya wengine wote na ilikuwa ni faraja sana. Baba yake Muislam mama yake Mkristo, nakumbuka sana alivyokuwa ananipigia simu usiku tu saa kumi mfano, na kunambia tusali, sala nishaisahau ila ilikuwa napenda sana kwa kuwa yeye si Mkristu. Ile sala ya ya kulala ya kikatoliki dah siamini nimeisahau. Nitakwambia imenitoka tu coz umeniuliza ghafla
Nachokumbuka pia ni kuwa alinipa usichana wake, ila mapenzi yalikuwa kama movie kipindi kile, baada ya miaka miwili alibadilika sana
Nimekosa hata mood ya kuandika kwa kusahau ile sala