Kwako madam President: Watu wasipokuelewa basi jaribu kuwaelewa

Kwako madam President: Watu wasipokuelewa basi jaribu kuwaelewa

toobiter

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2017
Posts
1,441
Reaction score
2,877
Kuna mtu aliwahi kusema
"A great man shows his greatness by the way he treats little men"

-Wewe ndiyo "great man" kwa sasa na hilo hakuna namna ya kulikwepa kulikiri.
-Kwa sasa Kila mtu anasubiri kuona how you treat your "little men"


Sio kwa tusi,kwa kashfa au dhihaka ila ni kwa kanuni ya mantiki(logic).
Muda huu jitahidi saana kutumia AKILI badala ya MOYO.
-Sisemi ni rahisi kwa yaliyotokea,hapana.Ila kama taifa tunahitaji kupona na tunahitaji "mponyaji" na hatua nzuri za "uponyaji".

Kama taifa tuko mahala ambapo hatujawahi kuwa,Raia wanazidi kupoteza Imani na vyombo vyao vya usalama(majeshi yote) na pia wanapoteza Imani na vyombo vya kutoa haki na mifumo yake(Mahakama)

-Tunaweza kupuuzia hili na kuendelea na style yetu kama kawaida yetu ila "MUDA" ni mwalimu mzuri ila anafundisha kwa gharama kubwa na maumivu makubwa sana.

Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Nchi yetu.salaam
 
Back
Top Bottom