Kwako Mkurugenzi mpya, BRELA mnafukuza wawekezaji

Kwako Mkurugenzi mpya, BRELA mnafukuza wawekezaji

Janja PORI

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2011
Posts
825
Reaction score
246
Mwaka 2020 umeanza na fumua fumua ya hali ya juu pale BRELA lakini kwetu wadau wa BRELA na wadau wa wawekezaji tunaona ndiyo kwanza kero imeanza.

Wakati wa KAKWEZI japo BRELA kulikuwa na urasimu na baadhi ya madudu lakini angalu mambo yalikuwa yanaenda, kwa sasa kusajili KAMPUNI Tanzania kwa njia ya mtandao ya kupasa uweke mwezi mzima, utaambiwa:

a) Mfumo upo kwenye matengenezo
b) Maombi yapo FINAL DECISION; hii ni kero kuanzia mwaka 2020 uanze kuitatua
c) Uelewa wa masuala ya makampuni na kodi ni mdogo sana sana kwa watumishi pale BRELA

MKURUGENZI MPYA TUNAOMBA ZINGATIA HAYA ILI KUENDANA NA KASI YA UWEKEZAJI NCHINI

1. Ondoa kasumba ya watu kuajiriwa kwa kujuana, najua wewe umetoka BoT hebu jaribu kufanya BRELA iwe na watu wenye brain kidogo kama TRA, BOT etc

2. Anzisha mafunzo (Mafunzo endelevu) kwa vijana wako, kusema kweli wengi hapo hata Company Law (sheria wanayosimamia kila siku) hawaijui. Kuna mawakili wako kwenye practice kwa muda sasa, jaribu kuwaomba waje watoe mafunzo hapo BRELA kuboresha utendaji.

3. Anzisha mafunzo au seminar za Corporate Management and Tax Implications, vijana wako wajue implications za any changes to a company na mambo ya kodi na athari katika uchumi. Naona hapo BRELA mnamtegema Seka kila kitu, huyo Seka yuko busy sana; tafuta watu smart wa kumsaidia, kumbuka BRELA ndo kitovu cha biashara nchini.

4. Boresha mfumo wako ORS, bado una mapungufu mengi sana, sana. Mfano, leo hii mtu akitaka kubadili MEMART ya kampuni yake bado hamna standard nini kifanyike. Kampuni ikiwa na shareholder public haiwezi kwenda online, kampuni ikiwa na shareholder ambaye sio individual au company mfano NGO haiwi accomodated etc.

5. Kutana na wadau hasa Mawakili na Accountants wakusaidie kutatua changamoto, mwenzako Kakwezi alifanikiwa kwenye hili.

6. Rudisha utumishi wafanyakazi wala rushwa na wasio jua kitu zaidi ya kuleta ukiritimba, na dharau.

7. Hebu ifanya BRELA iwe na hadhi ya BoT, ndo maana umewekwa hapo kwa kazi maalumu.

8. BRELA inaweza kuwa kitovu kikubwa cha ukwepaji wa kodi hasa usipokuwa na lawyers makini katika masuala ya company structure and restructure.

8. Kama kuna tatizo kwenye mfumo, hebu toeni taarifa kwa wadau.

Asante.
 
Ukitaka kucheka mpaka ufe, tembelea hiyo website yao sasa; sidhani kama imetengenezwa na mtu anayejua hata HTML, yaani haiko user friendly kabisa na inabagua vifaa na vivinjali kiuweli ni zaidi ya aibu taasisi muhimu kama hii kuwa na website ya aina hii.
 
embu tusaidie mkuu maana naona unauelewa wa haya mambo.Mimi na kijana mwenzangu hapa tumejikusanya wee tuanzishe business sasa shughuli imekuwa kusajili jina,yan tangu mwaka jana mwez wa 12 mpaka leo bado tunasajili jina yani majina zaidi ya sita yote yanakataliwa unaambiwa yamefanana ila mengine ni yapo unique kweli kweli.Naomba mwenye uelewa na haya mambo anielezee kidogo,au kuna namna maana bongo kuna mambo hayaend kama uko nje ya reli
 
Majina ya Kampuni kukataliwa Ni kero kubwa mno na usumbufu. Sababu kubwa Ni kuwa BRELA hawajaweka wazi criteria za jina la Kampuni kukubalika. Inatakiwa waseme jina linatakiwa kuwa similar chini ya % ngapi?

Brela wanasema name of Company will be on final decision of Brela. Kwa hiyo wamejipa nafasi wao kuamua.
 
embu tusaidie mkuu maana naona unauelewa wa haya mambo.Mimi na kijana mwenzangu hapa tumejikusanya wee tuanzishe business sasa shughuli imekuwa kusajili jina,yan tangu mwaka jana mwez wa 12 mpaka leo bado tunasajili jina yani majina zaidi ya sita yote yanakataliwa unaambiwa yamefanana ila mengine ni yapo unique kweli kweli.Naomba mwenye uelewa na haya mambo anielezee kidogo,au kuna namna maana bongo kuna mambo hayaend kama uko nje ya reli
Nadhani inabidi u'search jina unalotaka kusajili kwanza kabla ya kusajili ili uone yaliyopo kwanza
 
Naona hapa shughuli ni ndefu,maana kwenye system zao zinakuwa zinasumbua sana lakin ukienda pale upate mrejesho unashangaa baada ya dk kadhaa wanakwambia name rejected

Huu Ni mwanya wa Rushwa

Brela hawaweki wazi criteria za kujua jina lipi litakupalika. Katika name search, Kuna %. Na hawaweki wazi kuwa jina litakupalika kwa % ngapi. Wanasema name will be accepted under final decision of Brela.
 
Napata wapi list ya majina yaliyosajiliwa ili kuhakiki?
Katika option za ku'search name hapo kwenye website ya brela

weka jina unalotaka kusaliji
Yatakuja yanayokaribia fanana la hilo la kwako
Hivyo itabidi uchague na usajili ambalo halipo

wenye uzoefu zaidi watasema
 
Back
Top Bottom